1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wakiislamu washambulia makazi ya rais na uwanja wa ndege

9 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EYv0

BAIDOA

Wanamgambo wa mahakama za kiislamu nchini Somalia wameshambulia makaazi ya rais pamoja na Uwanja wa ndege katika mji wa Baidoa ambako ni makao makuu ya serikali ya mpito.Mwanajeshi mmoja aliuwawa na wengine sita wakajeruhiwa.

Shambulio hilo ni la kwanza katika mji huo wa Baidoa tangu mwaka 2006 baada ya wanajeshi wa serikali wakisaidiwa na vikosi vya wanajeshi wa Ethiopia kuwatimua wanamgambo wakiislamu katika eneo la kusini na kati mwa nchi hiyo.

Kundi la wanamgambo wa Shabaab limedai kuhusika na shambulio hilo,msemaji wake Robow Abu Mansor amesema Baidoa ndilo eneo pekee ambalo limesalia kuwa ngome ya wanajeshi wa Ethiopia na vibaraka wake serikali ya mpito kwa hivyo wapiganaji wa kundi hilo hawana budi kuwamaliza.Kundi hilo limesema litaendelea kuwalenga wanajeshi wote wakigeni pamoja na wafanyikazi wengine walioko nchini humo.