1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamaji wa Uengereza wanaweza kuuza hadithi za kifungo chao nchini Iran

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBS

London:

Wanamaji wa Uengereza walioachiwa huru wanaweza kuviuzia vyombo vya habari usimulizi wa maisha yao ya zaidi ya wiki moja kifungoni.Kwa kufanya hivyo wizara ya ulinzi ya Uengereza inaachana na desturi za kawaida za kijeshi.Msemaji wa wizara ya ulinzi anasema imeamuliwa hivyo kwasababu ya kiu kikubwa cha vyombo vya habari kutaka kujua nini hasa kimetokea wanamaji hao walipokua wakishikiliwa nchini Iran.Iran inahoji wanamaji hao wamekamatwa kwasababu wameingia bila ya ruhusa katika eneo la bahari.Baada ya kurejea nyumbani wanamaji hao wanadai lakini walilazimishwa kuridhia.