1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa serikali iliyoangushwa Mali wateswa

31 Julai 2012

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty International limesema wanajeshi watiifu kwa serikali iliyoangushwa Mali wameteswa na haki zao nyingine kukiukwa mikononi mwa jeshi lililofanya mapinduzi.

https://p.dw.com/p/15gwy
Malian junta soldiers patrol a road in Kati, outside Mali's capital Bamako, April 1, 2012. Mali's junta leader promised to reinstate the constitution from Sunday, hours before a deadline set by West African neighbours to start handing over power, and as rebels encircled the ancient trading post of Timbuktu. Amadou Sanogo, who led a military coup on March 22, also pledged to re-establish all state institutions before organising a transfer of power back to civilians through democratic elections. REUTERS/Luc Gnago (MALI - Tags: MILITARY POLITICS)
Mali Bamako SoldatenPicha: Reuters

Katika ripoti iliyotolewa leo nchini Ufaransa, shirika hilo limesema wanajeshi hao aidha walitoweka au kuuawa mbali na kuteswa wakati walipowekwa kizuizini baada ya kushiriki katika jaribio jingine la tarehe 30 Aprili kutaka kulipindua jeshi lililokuwa limeiondoa serikali ya kiraia mnamo Machi 22.

Ripoti hiyo ya Amnesty International, ambayo inakuja siku kumi baada ya ujumbe wa kutathmini hali halisi nchini Mali mnamo mwezi Julai, ina matukio ya visa vya ukiukaji wa haki za binaadamu vilivyofanywa na wanajeshi watiifu kwa uongozi wa kijeshi dhidi ya wanajeshi na polisi waliohusishwa na mapinduzi ya pili ya kuliondoa jeshi.

Wangambo wametwaa udhibiti wa upande wa Kaskazini mwa Mali
Wangambo wametwaa udhibiti wa upande wa Kaskazini mwa MaliPicha: Reuters

Shirika hilo limewataka maafisa wa Mali kusitisha vitendo vya ukiukaji wa haki za binaadamu na kuanzisha uchunguzi kuhusu visa kadhaa vya kutoweka kwa watu, mauaji ya kiholela na mateso.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Hayo yanajiri wakati rais Traore akikabiliwa na muda wa mwisho leo uliowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo inatarajiwa kuweza kukabiliana na uvamizi wa upande wa kaskazini uliofanywa na wanamgambo wa kiislamu wenye misimamo mikali.

Mara baada ya wakati mmoja kuwa nchi dhabiti kidemokrasia katika eneo hilo, nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilitumbukia katika mgogoro katika nusu ya mwaka wakati waasi wa Tuareg walipofanya mapinduzi ambayo yaliwakubalia wanamgambo kutwaa zaidi ya nusu ya nchi hiyo kwa upande wa kaskazini.

Jeshi hilo likiongozwa na Kapteni Amadou Sanogo lilimwondoa madarakani Amadou Toumani Toure mnamo tarehe 22 mwezi Machi, na kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito ya kiraia, ambapo Rais wa mpito Dioncounda Traore alichaguliwa kuiongoza mwezi Aprili.

Wangambo wametwaa udhibiti wa upande wa Kaskazini mwa Mali
Wangambo wametwaa udhibiti wa upande wa Kaskazini mwa MaliPicha: Reuters

Wanachama wa Amnesty waliwahoji watu 50 waliowekwa kizuizini katika kituo rasmi, ambao awali walikuwa wakizuiwa katika mazingira mabaya katika kambi ya kijeshi .

Wafungwa hao walisema walishuhudia watu 21 wakitoweka baada ya kuondolewa katika vyumba vyao vya gereza katika usiku wa terehe 2 na 3 mwezi Mei.

Pia walieleza kuhusu mazingira ya kudhalilisha na hata vitendo vya mateso na kuingiliwa kingono .Mfungwa mmoja alinukuliwa akisema katika ripoti hiyo ya Amnesty kuwa mmoja wa wanajeshi aliingiza virungu midomoni mwao, kuwazuwia kuongea.

Shirika hilo limezitaka Mahakama nchini Mali kuanzisha haraka uchunguzi kuhusu madai haya na kurejesha utulivu katika nchi hiyo ambayo wananchi wake wameathirika sana katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman