1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wafanya maandamano kusisitiza ulinzi wa mazingira.

9 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZGl

Berlin. Wanaharakati wa ulinzi wa mazingira wamekuwa wakifanya maandamano katika miji zaidi ya 50 duniani kote ikiwa ni sehemu ya hatua ya siku ya mazingira duniani. Katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin , kiasi cha watu 5,000 walisimama mbele ya lango kuu la Brandenburg, wakitoa wito wa upunguzaji mkubwa wa gesi zinazoharibu mazingira.

Jana Jumamosi jioni nyumba na ofisi katika sehemu nyingi za Ujerumani zilizimwa taa kwa muda wa dakika tano kuonyesha matumizi mabaya ya umeme. Taa katika lango la Brandenburg pamoja na kasri maarufu la Bavaria Neuschwanstein pia zilizimwa.