Wanafunzi wajifunza Kijerumani mapumzikoni | Masuala ya Jamii | DW | 20.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Wanafunzi wajifunza Kijerumani mapumzikoni

Je,wanafunzi wenye bidii hufanya nini wakati wa mapumziko,ikiwa somo mojawapo linahusika na lugha ya Kijerumani?

Chuo Kikuu cha kale cha Heidelberg,ambacho mwaka 1986 kilisherehekea miaka 600 tangu kuanzishwa kwake

Chuo Kikuu cha kale cha Heidelberg,ambacho mwaka 1986 kilisherehekea miaka 600 tangu kuanzishwa kwake

Bila shaka watataka kupiga msasa ujuzi wao wa lugha hiyo.Na wapi pa kufanya hivyo vizuri zaidi isipokuwa katika Chuo Kikuu cha kale kinachoheshimiwa katika mji wa Heidelberg.

Katika mwezi wa Agosti wanafunzi 600 kutoka nchi 60 hukusanyika pamoja katika Chuo Kikuu cha Heidelberg kushiriki katika kozi ya kujifunza lugha ya Kijerumani ambayo kwa desturi hutolewa wakati wa mapumziko.

Kozi hiyo ya kimataifa inatolewa na Chuo Kikuu cha Heidelberg tangu miaka ya ishirini ya karne iliyopita.

Katika miaka hiyo ya ishirini,kozi ya kujifunza Kijerumani ilianzishwa kwa kuwa na wanafunzi 60 kutoka Marekani na wengi wao waliishi pamoja na maprofesa majumbani mwao.

Siku hizi,wanafunzi wanatoka sehemu mbali mbali za dunia,kushiriki katika awamu tatu za mafunzo ya lugha,michezo ya kuigiza au kuchapisha magazeti.Baadhi kubwa ya wanafunzi hao huja zaidi ya mara moja kama wageni wa mji wa Heidelberg katika majira ya joto.Kozi hiyo inayotolewa wakati wa mapumziko inasifiwa na kuheshimiwa kama ni mfano bora wa kubadilishana wanafunzi.

Kwa maoni ya mratibu wa kozi hiyo ya mapumzikoni,Almuth Bofferding,kozi hiyo ni kiini cha idara ya Ujerumani ya kubadilishana wanafunzi katika vyuo vikuu.Anasema,katika kipindi cha miaka 81 tangu kuanzishwa kwa masomo ya aina hiyo,idadi ya wanafunzi imeongezeka kwa mara kumi.

Kozi hiyo ya majuma manne hugharimu Euro 470,hiyo ikiwa ni pamoja na gharama za usafiri.Mwanafunzi anahitaji Euro 300 zingine kulipia mahala pa kuishi.Mwaka huu,kundi kubwa kabisa la wanafunzi limetoka China.

Kwa wastani,kama wanafunzi 10 kutoka jumla ya hao 600,wanapomaliza kozi ya Kijerumani,huamua kuendelea kusoma katika Chuo Kikuu cha Heidelberg.