1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanafunzi wafyatuliwa risasi Marekani

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaSA

LAS VEGAS:

Nchini Marekani,wanafunzi 6 wamepigwa risasi walipokuwa wakiteremka basi lao la shule katika mji wa Las Vegas.Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, wanafunzi 2 wamo katika hali mbaya sana. Inaaminiwa kuwa si chini ya watu wawili walihusika katika mashambulizi hayo.