1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamisri wapiga kura

16 Juni 2012

Wamisri wameanza kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo kati ya mgombea anayefuata siasa zinazoegemea dini ya Kiislamu dhidi ya waziri mkuu wa zamani wa utawala wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/15GGr
ARCHIV - Die Kandidaten zur Präsidentenwahl in Ägypten, der Islamist Mohammed Mursi (l./Foto vom 17. Mai 2012) und der frühere Mubarak-Minister Ahmed Schafik (Foto vom 14. Mai 2012). Bei der Präsidentenwahl in Ägypten läuft es auf eine Stichwahl zwischen dem Islamisten Mohammed Mursi und dem früheren Mubarak-Minister Ahmed Schafik hinaus. Ein Mitglied der Wahlkommission sagte am Freitag (25.05.2012) in Kairo, die beiden Politiker lägen nach der Auszählung von 90 Prozent der Stimmen mit Abstand vor den Mitbewerbern. Das offizielle Ergebnis der Wahl werde erst am Sonntag (27.05.2012) veröffentlicht, fügte er hinzu. EPA/KHALED ELFIQI (zu dpa 1012 am 25.05.2012) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Präsidentenwahl in Ägypten Mohammed Mursi und Ahmed SchafikPicha: picture-alliance/dpa

Zoezi hilo linafanyika huku kukiwa na hali ya wasiwasi na wakati hali kisiasa baada ya mageuzi haieleweki.

Ahmed Shafiq, waziri mkuu wa mwisho wa rais alieondolewa madarakani Hosni Mubarak anapambana na mgombea wa chama cha Udugu wa Kiislam, Mohammed Mursi katika zoezi la kupiga kura litakalodumu kwa siku mbili ambapo kiasi ya raia milioni 50 wamejiandikisha kushiriki zoezi hilo.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema asubuhi ambapo kiasi ya askari 150,000 wametawanywa kwa nia ya kudhibiti hali ya usalama kwenye uchaguzi huo wenye mgawanyiko mkubwa. Kinyang'anyiro hicho kimeleta mtengano na hasa kwa wale wenye hofu ya kurejea madarakani kwa uongozi wa zamani kupitia Shafiq na wale wanaotaka kutenga siasa na dini na shaka kwamba chama cha Udugu wa Kiislamu kitavuruga uhuru wa watu.

Vituo vya kupiga kura vilifungulwia mapema leo kote Misri
Vituo vya kupiga kura vilifungulwia mapema leo kote MisriPicha: Reuters

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo Mursi alipata asilimia 24.7 ambapo Shafiq ambae pia alikuwa kamanda wa jeshi la anga alipata asilimia 23.6 ya kura.

Uchaguzi huo unakuja huku kukiwa na hali ya vurugu ambalo linaweza kusababisha uongozi wa kijeshi, ambao ulichukua madaraka wakati rais Hosni Mubarak alipojiuzulu Febrauri mwaka jana, inaendelea kuimarisha nguvu zake madarakani.

Alhamis wiki hii, mahakama kuu ya katiba nchini humo ilitoa hukumu kwa baadhi ya vipengee katika sheria inayoongoza uchaguzi wa bunge kuwa ni batili, hii ikiwa ni kulivunja bunge linalodhibitiwa na makundi ya Kiislamu.

Chama cha ugudu wa Kiislamu kilipata asilimia 47 ya viti katika hatua ya mpambano kati ya mwezi Novemba mwaka jana na Februari mwaka huu.

Waandamanaji Misri wakipinga umauzi wa kumkubalia Ahmed Shafiq kushiriki uchaguzi
Waandamanaji Misri wakipinga umauzi wa kumkubalia Ahmed Shafiq kushuriki uchaguziPicha: dapd

Mahakama hiyo ya juu pia imetoa hukumu kuwa sheria inayowatenga baadhi ya wanasiasa kuwa ni kinyume na katiba, sheria ambayo inawazuwia maafisa waandamizi wa utawala wa mubarak pamoja na wanachama wa ngazi ya juu wa chama ambacho hivi sasa kimefutwa kutogomea wadhifa wowote wa uongozi nchini humo kwa muda wa miaka 10. Sheria hiyo , iliyopitishwa na bunge mapema mwaka huu, imetishia kumzuwia Shafiq kugombea uongozi.

Vyama vya siasa nchini Misri pamoja na wanaharakati wamelishutumu baraza kuu la uongozi la majeshi ya ulinzi kwa kufanya mapinduzi, baada ya hatua kadha ambazo zinaimarisha madaraka yake kabla ya uchaguzi. Uamuzi huo wa Alhamis wiki hii umekuja siku moja baada ya uamuzi wa wizara ya sheria kuwapa wanajeshi haki ya kuwakamata raia baada ya uwezo huo kuondolewa wakati sheria ya hali ya hatari iliyodumu kwa muda wa muongo mmoja kumalizika muda wake hapo Mei 31.

Mwandishi : Sudi Mnette /afpe
Mhariri: Sekione Kitojo