1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakulima wa Afrika wapatiwa dola milioni 13

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbL3

JOHANNESBURG

Kundi la kilimo linaloongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan limetowa dola milioni 13 katika ruzuku kusaidia biashara ndogo ndogo nchini Tanzania,Kenya na Malawi ili kupunguza bei za pembejeo za kilimo katika juhudi za kuongeza mazao ya kilimo.

Wafanya biashara wadogo wadogo wa reja reja watauza pembejeo kama vile mbegu,mbolea na zana za kilimo kwa familia za vijijini milioni moja na laki sita kutakakowanufaisha wakulima milioni nane na laki nane na familia zao katika nchi hizo tatu.

Taarifa ya kundi hilo la kilimo imesema leo hii ukosefu wa pembejeo muhimu za kilimo umefanya iwe haiwezekani kabisa kwa wakulima wadogo wadogo kuongeza mavuno yao au kipato chao na hiyo kuzidi kukomelea umaskini uliotopea.

Kundi hilo linalojulikana kama Muungano wa kuleta Mapinduzi ya Kilimo Afrika AGRA umesema mipango ya serikali ya nchi hizo inakusudia mapato ya wafanyabiashara wadogo vijijini kwa asilimia 30 na kupunguza bei za pembejeo kwa asilimia 15 katika kipindi cha miaka mitatu.