1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakenya wajitokeza kwa wingi kuipigia kura katiba mpya

Josephat Nyiro Charo4 Agosti 2010

Zoezi la kuhesabu kura latarajiwa kuendelea usiku kuhca huko Bomas jijini Nairobi, huku tume ya uchaguzi ikitangaza matokeo baada ya kila dakika 60

https://p.dw.com/p/Oc6C
Wakenya wakipigia kura katiba mpya iliyopendekezwaPicha: AP

Nchini Kenya shughuli ya kuipigia kura ya maoni rasimu ya katiba mpya imekamilika.Lengo la kura hiyo ni kuiidhinisha au kuipinga rasimu ya katiba mpya.Zoezi hilo ni sehemu ya mageuzi ya kisiasa yaliyo na azma ya kuzuwia ghasia kutokea kama ilivyokuwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba mwaka 2007.Usalama uliimarishwa kote nchini na kwa sasaTume ya muda ya uchaguzi inajiandaa kuanza awamu ya pili ya shughuli hiyo ya kuzihesabu kura.Wakati huu maafisa wa Tume hiyo watatumia mitandao ya kompyuta na simu za mkononi kuzihesabu kura zilizopigwa.Mwandishi wetu wa Nairobi Afred Kiti alipita mitaani na kutuandalia ripoti ifuatayo.