1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakatalani wapiga kura kutaka kujitenga na Uhispania

Sekione Kitojo
1 Oktoba 2017

Polisi wa kuzuwia ghasia waliingia kwa nguvu vituo vya kupigia kura katika jimbo la Catalonia Jumapili(01.10.2017)wakipora masanduku na karatasi za kura wakizuwia kura ya maoni, serikali ikionesha mamlaka yake.

https://p.dw.com/p/2l3mg
Spanien Referendum Katalonien Wähler
Picha: Getty Images/AFP/J. Lago

Polisi  walivunja  milango kwa  nguvu  na  kuingia  katika  vituo vya kupigia  kura  wakati wakatalani  ambao  wameonesha  ukaidi wakipiga  kelele "majeshi  ya  uvamizi yaondoke!" na  kuimba  wimbo wa  taifa  wa  jimbo  hilo tajiri  la  kaskazini  mashariki  mwa  nchi hiyo. Katika  tukio  moja  mjini  Barcelona, polisi walifyatua  risasi  za mipira.

Spanien Katalonien Unabhängigkeits-Referendum Poilzei schreitet ein
Polisi wakimuondoa kwa nguvu mwanamke mzee kutoka kituo cha uchaguziPicha: Getty Images/D. Ramos

Kura  hiyo  ya  maoni , iliyotangazwa  kuwa  ni kinyume  na  sheria na  serikali  kuu  mjini  Madrid, imeiweka  nchi  hiyo katika  mzozo mkubwa  kabisa  wa  kikatiba katika  muda  wa  miongo  kadhaa  na kusababisha kujitokeza  zaidi mtengano  wa  karne  nyingi  kati  ya Madrid  na  Barcelona.

Licha  ya  hatua  hizo  za  polisi, mamia ya  watu  walijitokeza  katika milolongo  mirefu  katika  miji  na  vijiji  katika  jimbo  hilo  kupiga  kura zao. Katika  kituo  kimoja  cha  kupigia  kura  mjini  Barcelona, watu wazima na wanawake  wenye  watoto  waliingia  kwanza.

"Nina furaha  kubwa  kwasababu  licha  ya  vikwazo  vyote vilivyowekwa, nimefanikiwa  kupiga  kura," amesema  Teresa , mstaafu  mwenye  umri  wa  miaka  72 mjini  Barcelona ambaye alisimama  katika  msitari kwa  masaa  sita.

Spanien Referendum Katalonien Polizei
Polisi wa kuzuwia ghasia wakiingia katika kituo cha kupigia kuraPicha: Getty Images/AFP/L. Gene

Kura  hiyo  haitakuwa  na  uhalali  wa  kisheria kwa  kuwa  imepigwa marufuku  na  mahakama  ya  katiba  ya  Uhispania , na serikali  kuu mjini  Madrid kwa kukiuka  katiba  ya  mwaka 1978.

Wachache wapendelea kujitenga

Idadi  ndogo  ya  watu  kiasi  ya  asilimia 40 ya  Wakatalani wanaunga  mkono  kura  ya  maoni, uchunguzi  wa  maoni  ya wapiga  kura unaonesha, licha ya  kuwa  idadi  kubwa  ya  watu wanataka  kura  hiyo  ya  maoni  ifanyike kuhusiana  na  suala  hilo. Jimbo  hilo lenye  wakaazi milioni 7.5 lina  uchumi mkubwa  kuliko ule wa  Ureno.

Polisi 11  tisa  kutoka  jeshi la  taifa  la  polisi  na  wawili  kutoka katika  kikosi  cha  ulinzi  wa  umma  wamejeruhiwa wakati wakijaribu  kuzuwia kura  hiyo  ya  maoni  iliyopigwa  marufuku katika  jimbo  la  Catalonia.

Pia baadhi  ya walinzi  hao wa umma , "wakiponyoka haraka" wakikimbia  na  gari  yao kutoka  katika  kundi la watu  waliokuwa wakiirushia  mawe  gari  hiyo katika  eneo la  Saint Carles de la Rapita, kiasi  ya  kilometa  180 kusini  magharibi  mwa  Barcelona.

Wizara  ya  mambo  ya  ndani  ya  Uhispania  imetoa  taarifa  hizo kupitia  mtandao  wa  Twitter, baada  ya  maafisa  wa  afya  jimboni Catalonia  kusema wapiga kura 38 wamejeruhiwa  kufuatia mapambano  na  "polisi  wa  Uhispania," ikiwa  ni  pamoja  na  tisa ambao  wamepelekwa  hospitali.

Spanien Referendum Katalonien Polizei
Wananchi wakinyanyua mikono juu baada ya polisi kukamata masanduku ya kuraPicha: Getty Images/AFP/P. Barrena

Mbunge  wa  bunge  la  Israel  anayeangalia  kura  hiyo  ya  maoni ya  kudai  uhuru  jimboni  Catalonia  amesema  ameshitushwa na polisi  wa  Uhispania  kutumia   risasi  za  mipira  dhidi  ya  makundi ya  watu  ambao  hawana  silaha. Ksenia svetlova  amesema leo Jumapili (01.10.2017) kwamba  risasi  zilizotumika "zinaweza kuvunjavunja kichwa  cha  mtu," amesema  hakutarajia  kuona  mbinu kama  hizo barani  Ulaya.Amesema  ameona  watu  wakivuja  damu na  waliojeruhiwa katika  tukio  hilo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape / rtre

Mhariri: Hamidou , Oummilkheir