1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajerumani 2 na Mholanzi waachiliwa huru Kenya

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuqG

NAIROBI: Wajerumani 2 waliokamatwa nchini Kenya, wameachiliwa huru.Mwanamuziki Andrej Hermlin aliekamatwa wakati mmoja na Mjerumani mwenzake na Mholanzi hapo siku ya Alkhamisi,amezungumza kwa simu na shirika la habari la AFP.

Watu hao 3 walikamatwa na polisi ya Kenya kwa kushukiwa ugaidi.Hermlin na mpigapicha wa Kijerumani walikuwa nchini Kenya kutayarisha ripoti ya usafiri kwa niaba ya jarida moja la Berlin.Raia wa Uholanzi aliekamatwa,alitaka kutengeneza filamu juu ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya,Raila Odinga.