1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waholanzi wawili, wajiunga na Bundesliga

31 Agosti 2012

Dirisha la shughuli za kuwasajili wachezaji kwa msimu huu lilifungwa jana usiku huku vilabu vikifanya usajili wa dakika za mwisho mwisho wa wachezaji wapya ili kuimarisha makali yao.

https://p.dw.com/p/161fd
Netherlands' Ibrahim Afellay reacts after he missed an opportunity to score during their Group B Euro 2012 soccer match against Denmark at the Metalist stadium in Kharkiv, June 9, 2012. REUTERS/Yves Herman (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
EURO 2012 Fußball Niederlande Dänemark Gruppe BPicha: Reuters

Hapa Ujerumani mshambuliaji wa timu ya Uingereza Tottenham Hot Spurs Rafael van der Vaart alisajiliwa na klabu ya Hamburg. Nyota huyo wa Uholanzi alikuwa na misimu miwili mfululizo uanjani White Heart Lane, lakini akaelezea hamu yake ya kurejea katika klabu ambayo alimaliza miaka mitatu kabla ya kuhamia Real Madrid. Nayo klabu ya Schalke 04 jana ilimsaini mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Ibrahim Affelay kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Barcelona. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusiana na usajili wa kiungo huyo mshambuliaji.

Droo ya Ligi ya Mabingwa
Chelsea wataanza harakati za kutetea kombe la Ligi ya Mabingwa waliloshinda kwa mshangao msimu uliopita kwa mchuano wa kundi E dhidi ya mabingwa wa zamani Juventus uwanjani Stamford Bridge.

Droo ya mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa Ulaya ilafinyiwa mjini Monaco, Italia
Sherehe ya Droo ya mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa Ulaya ilafinyiwa mjini Monaco, ItaliaPicha: Reuters

Mabingwa hao wa Italia walionyanua kombe la Ulaya mara mbili, wataipa Chelsea mtihani mkali tarehe 19 Septemba kabla ya vijana hao wa Roberto di Matteo kupambana na wageni wa ligi hiyo FC Nordsjaelland wa Denmark na mabingwa wa Ukraine Shakhtar Donetsk.

Kundi D hatahivyo ndilo gumu huku kukiwa na mabingwa mara tisa wa Ulaya Real Madrid, mabingwa wa Uingereza Manchester City, mabingwa wa Ligi ya Uholanzi Ajax Amsterdam na mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund…

Bayern Munich walioshindwa na Chelsea katika fainali ya msimu uliopita kwa mikwaju ya penalti katika uwanja wao wenyewe wa Allianz Arena, watapambana na Valencia, Lille na BATE Borisov ya Belarus katika kundi F.

Barcelona, watakutana na mahasimu wao wa jadi Benfica, Spartak Moscow na Celtic. Nao Manchester United ambao ni mabingwa mara tatu wa Ulaya wa wamepangwa kupambana na Braga, Galatasaray na CFR Cluj. Montpellier wamepangwa kuchuana na Arsenal, Schalke 04 na Olympiakos.

Andres Iniesta aliwapiku Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika taji la mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya
Andres Iniesta aliwapiku Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika taji la mchezaji bora wa mwakaPicha: AP

Paris St Germain watapambana na Porto, Dynamo Kiev na Dinamo Zagreb. Kinyang'anyiro hicho kinaanza Septemba 18 na 19 huku awamu ya mechi za makundi ikikamilika wiki ya kwanza ya Desemba.

Katika habari nyingine za ulaya wiki hii mchezaji wa timu ya taifa ya Uhispania na klabu ya Barcelona Andres Iniesta alituzwa kuwa mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya.

Katika kura iliypigwa miongoni mwa waandishi habari 53 wa Ulaya, kiungo huyo wa Barca alimpiku mwenzake Lionel Messi na mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo. Messi alishinda tuzo hiyo msimu uliopita.

Iniesta ambaye aliifungia Uhispania bao la ushindi katika fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 na akapigiw akura kuwa mchezaji bora wa kinyag’anyiro cha UEFA EURO 2012, alipata kura 19, huku naye Messi na Ronaldo wakipata 17 kila mmoja.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/Reuters/AFP

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed