Wahariri watoa maoni juu ya Assad | Magazetini | DW | 11.01.2012
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Wahariri watoa maoni juu ya Assad

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani pia wasema Guantanamo ni aibu kwa sababu wafungwa wanawekwa kutokana na tuhuma tu na bila ya kufikishwa mahakammani

In this image made from video, Syrian President Bashar Assad delivers a speech in Damascus, Syria, Tuesday, Jan. 10, 2012. Assad gave his first speech Tuesday since he agreed last month to an Arab League plan to halt the government's crackdown on dissent. (Foto:Syrian State Television via APTN/AP/dapd) SYRIA OUT

Rais Bashar al-Assad wa Syria

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya hali ya nchini Syria na juu ya jela ya Guantanamo inayotimiza mwaka wa kumi.

Mhariri wa gazeti la Rhein-Necker anasema jela ya Guantamo inayosimamiwa na Marekani ni aibu.

Ni aibu siyo tu kwa sababu wafungwa wanateswa bali pia kwa sababu watu wanawekwa mahabusi katika jela hiyo kutokana na tuhuma tu. Hayo hayalingani hata kidogo na hadhi ya nchi kama Marekani.
Mhariri wa Flensburger Tageblatt anasema, katika kuadhimisha mwaka wa kumi tokea jela hiyo inanzishwe, umefika wakati wa kuleta haki.

Mhariri wa Flensburger Tageblatt anaeleza kuwa Rais Obama hakuweza kuitekeleza ahadi aliyoitoa hapo awali ya kuifunga jela ya Guantanamo,na kuondoa aibu ya Marekani katika kisiwa cha Kuba.

Lakini hayo yanaonyesha jinsi Rais wa Marekani anavyokuwa hana la kufanya pale ,bunge linapoamua kuzizuia sera zake.

Katika maadhimisho ya mwaka wa kumi wa kuwepo jela ya Guantanamo, pana ujumbe kwa bunge la Marekani. Sasa umefika wakati wa kuwatendea haki watu wasiokuwa na hatia ambao wamefungwa katika jela hiyo.

Gazeti la Nordwest linazungumzia juu ya hali ya nchini Syria. Mhariri wa gazeti hilo anakumbusha kwamba Rais Assad sasa anayapinga hata yale aliyoahidi kuyafanya hapo awali. Mhariri huyo anasema kuwa Assad alikuwa kiongozi alieingia madarakani kwa kuwapa watu wake matumaini. Lakini anasema hayo yalikuwa miaka 10 iliyopita. Lakini sasa zimebakia hadithi tu anasisitiza mhariri.

Anasena kuleta mabadiliko katika uongozi, siyo jambo rahisi nchini Syria.Hali ni tete nchini humo. Hakuna uwezekano wa Nato kuingilia kati kijeshi. Kwa sasa Rais Assad anaitumia hali ya wapinzani kwa manufaa yake. Lakini njama hizo hazitamsaidia kwa muda mrefu. Gazeti linasema utawala wa Assad utasambaratika au utapaswa kutambua ulazima wa kuleta mabadiliko.

Jana Rais Assad aliwahutubia watu wake na kudai kwamba upinzani dhidi ya utawala wake unatokea nje. Juu ya kauli hiyo mhariri wa gazeti la Financial Times Deutschland anasema kuwa hotuba hiyo ,ulikuwa uongo usiokuwa na mithili katika muda wote wa utawala wa Assad.

Wakati maalfu ya wananchi wake wanaupinga utawala wake, na wakati watu wa Syria wanakufa kila siku katika harakati za kuupinga utawala wa Assad Rais huyo anadai kwamba upinzani dhidi yake ni njama zinazotokea nje ya Syria. Lakini hhilo siyo jambo la kushangaza kwani tuliyashuhudia hayo kutoka kwa madikteta wengine katika nchi za kiarabu waliojongomea daima.

Mwandishi/Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen/Mhariri/

 • Tarehe 11.01.2012
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Maneno muhimu assad
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13hja
 • Tarehe 11.01.2012
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Maneno muhimu assad
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13hja