1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri wasema mtuhumiwa siyo kichaa

Abdu Said Mtullya21 Machi 2012

Wahariri wa magazeti wanatoa maoni juu ya mtuhumiwa wa mauaji ya mjini Toulouse na juu ya azimio kuhusu Syria.Wahariri hao wanasema siyo sawa kutamka kuwa mtuhumiwa ni kichaa

https://p.dw.com/p/14OTE
Polisi wa Ufaransa wameizingira nyumba ya mtuhumiwa wa mauaji ya mjini Toulouse
Polisi wa Ufaransa wameizingira nyumba ya mtuhumiwa wa mauaji ya mjini ToulousePicha: Reuters

Gazeti la "Frankfurter Rundschau" linasema mauaji yaliyofanyika kwenye shule ya Wayahudi katika mji wa Toulouse nchini Ufaransa hayatokani na kauli zinazotolewa na wanasiasa wa Ufaransa katika kampeni zao za uchaguzi.

Mhariri wa gazeti hilo anatilia maanani aliyoyasema Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gueant juu ya ubora wa ustaarabu wa nchi za magharibi. Pia mjumbe wa chama cha mrengo mkali wa kulia Le Pen amekua anabatuka juu ya nyama halal na, Rais Sarkozy ameanza kuzungumzia juu ya suala la wahamiaji katika kampeni yake ya uchaguzi.

Sarkozy ameahidi kupunguza idadi ya wahamiaji kwa nusu. Mhariri wa gazeti la "Frankfurter Rundschau" anauliza jee masuala hayo yanayozungumziwa katika kampeni za uchaguzi yanatosha kumfanya mtu alierukwa akili awaue watu wengine? Inapasa mtu ajihadhari sana juu ya kuelezea mwambatano wa matendo ya mtu na hali yake ya kiakili.

Gazeti la"Hamburger Abendblatt"pia linatahadharisha juu ya kumwita muuaji wa Toulouse kuwa ni kichaa! Gazeti hilo linaeleza kwamba kumwita muuaji huyo kuwa ni mtu aliechanganyikiwa kiakli siyo haki. Jamii za Ulaya zinapaswa kujichunguza ili kuyabainisha maradhi yanayozisibu. Tatizo la kuwaingiza wahamiaji fulani katika jamii za Ulaya haliwezi kupuuzwa barani. Pia ni lazima kuangalia kwa makini,na kutambua kwamba baadhi ya michakato ya kuwajumuisha wahamiaji katika jamii za Ulaya inaweza kusababisha chuki isiyokuwa na mfuniko.

Mhariri wa gazeti la"Reutlinger General-Anzeiger"anatoa maoni juu ya azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa Syria. Mhariri huyo anasema jumuiya ya kimataifa itafanikiwa kuleta suluhisho nchini Syria ikiwa pande zote zitashiriki. Mhariri huyo anasema waasisi wa azimio la Umoja wa Umoja juu ya Syria wanatumai kwamba Urusi itashirikiana na mataifa mengine.

Lakini uwezekano wa kufanikiwa kuleta suluhisho,katika msingi wa juhudi za mjumbe maalumu,Kofi Annan ni mdogo kwa sababu Rais Assad anasema kwanza analo jukumu la kuwashughulikia wale anaowaita magaidi. Na kwa upande wao wapinzani wa utawala wa Rais Assad wanatamtaka Rais huyo kwanza asimamishe mashambulio na ayarudishe majeshi yake kambini ili mazungumzo yafanyike. Kilichobakia sasa mhariri anasema ni kutumai kwamba Urusi itaubadilisha msimamo wake kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen/

Mhariri: Abdul-Rahman