1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri waizungumzia ripoti juu ya njaa duniani

14 Oktoba 2014

Wahariri waliowengi Ujerumani wamezungumzia janga la njaa linalotishia maisha ya mamilioni ya watu duniani,hasa kutokana na vita na majanga ya maradhi

https://p.dw.com/p/1DVLt
Bango linalotangaza juu ya hali ya njaa Sierra Leone
Bango linalotangaza juu ya hali ya njaa Sierra LeonePicha: picture-alliance/dpa

Gazeti la MittleDeutsche Zeitung linaandika;

Kwa hakika njaa inaongezeka kule ambako kumegubikwa na majanga kuanzia maradhi ya Ebola hadi Ukimwi. Lakini pia njaa inazidi kwenye maeneo hayo kutokana na kukosekana nia ya kupambana na tatizo hilo. Mhariri anaendelea kusema kwamba baadhi ya wakati kuna ukosefu wa elimu na wakati mwingine hakuna nia ya kisiasa ya waliowachache katika nchi husika. Nchi zinazoendelea zinaweza kwa sehemu fulani kuibadili hali hiyo ya zamani. Juu ya hilo lakini kuna sababu nyingine inayochangia njaa ambayo inatokana na nchi za magharibi,na sababu hiyo ni Vita.Mapigano nchini Iraq ni janga ambalo si tu la uvunjaji wa haki za binadamu.Kuna watu wengi ambao wanakosa hata mahitaji muhimu ya kila siku ambayo ni haki ya msingi. Haki ya kuishi.

Gazeti la Kölnerstadt Anzeiger linasema;

Ebola inatishia kusababisha janga kubwa la kiuchumi katika eneo la Afrika Magharibi na pengine bara zima kwa ujumla.Nchini Liberia na Sierraleone hakuna anayetaka tena kuekeza.Ni kusema Biashara na uzalishaji wa chakula unaweza kusimama.Ulimwengu kwahivyo unabidi kumulikia juu ya mapambano ya madaktari juu ya maradhi ya Ebola lakini pia juu ya mapambano dhidi ya njaa.

Mhariri wa Märkische Oderzeitung anasema;

Inatisha mtu kufikiria kwamba kuna watu wanaokosa chakula kila siku.Lakini tatizo hilo litapungua licha ya kwamba idadi ya watu inaongezeka. Hilo linawezekana na hasa rasilimali zikiwepo inawezekana kabisa njaa kuondoka. Nchi nyingi zinapiga taratibu hatua nzuri za maenedeleo.Lakini ni hatua zinazoonekana. Na kwa namna hiyo inawezekana kuwa na ulimwengu usiokuwa na njaa.

Kuhusu suala la vita vya kuuwania mji wa Kobane wahariri wamejishughulisha zaidi kuangalia kile kilichozungumziwa na chama cha upinzani nchini Ujerumani,chama cha Kijani,juu ya kutaka Ujerumani pia ipeleke wanajeshi wa ardhini kupambana na wanamgambo wa itikadi kali wa dola la Kiislamu.

Gazeti la Lausitzer Zeitung linasema

Chama cha Kijani Kama kundi dogo la upinzani si rahisi kugonga vichwa vya habari,ila pale kinnapozusha hoja ya uchokozi. Na kwahakika hilo ndilo lilikuwa lengo la hoja ya mwanasiasa wa chama hicho Göring-Eckardt. Suala la wanajeshi wa ujerumani kupelekwa katika vita vya ardhini nchini Syria na Iraq sio jambo linalozungumzwa hata kwenye vyumba vya mikutano seuze mbele ya macho ya ulimwengu.Na ndiyo sababu hata kauli ya waziri wa Ulinzi Ursula Von Der Leyen anayetokea chama cha CDU mbele ya umma ya kuitaka Ujerumani iweke kando miiko yake,ilizusha kauli za kumkosoa vikali

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman