Wageni wanaovumiliwa kukaa tu nchini | Masuala ya Jamii | DW | 09.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Wageni wanaovumiliwa kukaa tu nchini

Wageni wanaovumiliwa kuishi nchini Ujerumani hali zao karibuni zitatengenea ingawya kwa masharti.

Nchini Ujerumani kuna raia wa kigeni ambao wanavumiliwa tu kuishi bali hawana hadhi za ukimbizi.watu kama hawa kila wakati wanakuwa wamefunga virago vya tayari kuondoka nchni amri inapotoka kuwa hawavumiliw tena.

Idadi ya wakaazi wa aina hii humu nchini inafikia laki 2.

Waajiri wengi hawtaki kuwaajiri watu kama hawa ambao hawana uhakika iwapo kesho watakuwapo nchini au la.

Mawaziri wa ndani wa serikali za mikoa ya Ujerumani waliafikiana Novemba mwaka uliopita wale waliovumiliwa kwa miaka mingi sasa kuishi humu nchini,hati zao zigeuzwe na wapeewa hadhi ya kuwana wanabaki nchini endapo miongoni mwa mashari mengine wamepata kazi kujiendeshea maisha.

Kuna mkasa wa msichana mmoja alieitumia nafasi kama hiyo:

“Mwanzoni hali ilikua ngumu.Tukiishi katika hofu.kila barua inayokuja nyumbani,tukiifungua kwa wasi wasi,kwavile hatukujua iwapo wakati umewadia kufunga virago.”

Yildiz Kurter akizungumzia hapo hofu ya kuondoshwa nchini.Kwa miaka 15 aliihama uturuki na wazee wake.Kurta na jamaa zake ni wakristu wa Aramai na wakiandamwa nchini Uturuki kutokana na dini yao.

Hali ni hiyo,wakristu huko hawakuachiwa kuabudu dini yao kwa njia uhuru.Kwahivyo, ikawa ngumu kwetu kujiunga na wengine shuleni,kwavile tukitaka kun’gan’gania dini yetu na wao wakitaka kutulazimisha kuabudu dini yao.”

Tangu 1992 Yildiz na ukoo wake wakiishi karibu na mji wa Giessen,huko mkoani Hesse.Idara nayohusika na uhamiaji wa wageni nchini ikikataa kukukubali maombi yao ya ukimbizi.

Akina Kurter wakipewa tu haki ya kuvumiliwa kuishi na kila kwa mara kwa mwaka mmoja zaidi.Miaka 5 nyuma ilikua wasafirishwe kwa nguvu kurejeshwa Uturuki,lakini mwalimu wa watoto hao alisaidia kupitia malalamiko kuzuwia mpango huo.

Kuanzia hapo ikawa-ngojeni,ngojeni-ngoja mpaka lini ?.Yildiz akaanza masomo chuo kikuu-akitaka kusomea sanaa na kuwa mwalimuwa hesabu.Ombi lake la posho wakati akisoma likakataliwa.

Kurter asema kwamba, kwavile afisa alinuliza ninakaa vipi humu nchini na nikajibu navumiliwa tu-akasema la,haiwezekani.kwani nani atanirejeshea pia hizo ukiondoshwa nchini ?Kwahivyo, maisha hayakuwa rahisi kuishi chini ya hali ya kuvumiliwa tu.

Kuwa huku anasoma na kufanyakazi,haikuwezekana kwa Yildiz.Matumaini yakaja pale mawaziri wa ndani wa m ikoa walipopitisha azimio Novemba mwaqka jana kuwa wale wote wanaovumiliwa wana haki ya kubakia nchini endapo wamejipatia kazi za kufanya.

Hapo tena Yildiz akapewa hatia maalumu ya kuweza kufanya kazi.

“Nilianza kutafuta kazi na nikajipatia kazi katika shule m oja huko Giessen na tangu februari,mwaka huu nafanyakazi katika Sophie-Scholl-Schule.

Katika shule hiyo alijuana na Jana ambae ni kiwete anaendesha kigari.

“Unaweza kunambia ngapi 5 na 4 ? ni tisa.Barabara,baraba kabisa.Na mbili na 5? Saba.Barabara kabisa.Walimu katika shule hiyo ya Giessen wakimsaidia sana Yildiz kwani wakim,jua tangu pale akifanya mazuwezi shuleni humo.Kwa mfano wakipiga simu katika Idara ya uhamiaji wa wageni kuharakisha Yildiz anapatiwa hati ya ruhusa ya kufanyakazi.