1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa watoroka jela Kinshasa

18 Mei 2017

Uchunguzi unafanyika katika gereza kuu la mjini Kinshasa - Kongo ilikufahamu idadi ya wafungwa waliotoroka na madhara yaliosababishwa na shambulio la hapo jana

https://p.dw.com/p/2d9sS
Kongo Christlicher Sektenführer gewaltsam aus Gefängnis n Kinshasa befreit
Picha: picture alliance/AP/J. Bompengo

Duru zinaelezea kwamba watu wasiopungua sita waliuwawa akiwemo polisi mmoja, huku msako dhidi ya wafungwa waliotoroka akiwemo mbunge Ne Mwanda Nsemi unaendeshwa na polisi kwenye maneo kadhaa ya jiji la Kinshasa.

Ni vigumu kwa sasa kuelezea idadi kamili ya watu waliofariki na wale waliotorka kufuatia shambulizi la gereza kuu la Kinshasa. Waziri wa sheria na polisi hawajaelezea chochochote kuhusu hilo,huku wakiomba kusubiri matokeo ya uchunguzi. Kwenye taarifa fupi usiku a kumakaia leo msemaji wa polisi Pierrot Mwanamputu alisema kwamba msako dhidi ya mbunge Neamwanda Nsemi na watoro wengine unaendelea.Polisi ilitoa mwito kwa raia kuripoti kisa chochote cha mtu ama watu waliotoroka gerezani.

Msemaji wa serikali, Lambert Mende ambae ameomba uvumilivu katika kusubiri matokeo ya uchunguzi akitangaza  kwamba watu sita,washabuliaji watano na polisi mmoja waliuliwa kufuatia tukio hilo. Lakini mashahidi wameiambia DW kwamba zaidi ya wafungwa elfu tatu walitoroka gereza hilo la MAKALA, katikati mwa jiji la Kinshasa.

Viongozi wa serikali na Mashahidi tuliozungumza nao wanaelezea kwamba washambuliaji ni wafuasi wa kundi la kidini na la kisiasa la Bundu dia Mayala ambalo linaongozwa na Nemwanda Nsemi alieshikiliwa kwenye jela hilo toka mwezi machi. Waziri wa sheria Alexis Thambwe amesema kwamba kwa sababu za uchunguzi hawezi kutoa matokeo ya shambulizi hilo :

« Kunawathiriwa miongoni mwa walinzi wa gereza na vilevile wathiriwa miongoni mwa washambuliaji ambo ni wafuasi wa Ne Mwanda Nsemi. Kuna ushahidi tosha na Uchunguzi unaendeshwa na idara za kisusalama ».

Swali hivi sasa ni vipi shambulizi hilo lilifaulu wakati  ambapo  gereza kuu la kinshasa linaaminika kuwa moja wapo ya maeneo yaliona ulinzi mkali ?

« Tunaendesha uchunguzi, na kwa sababu za uchaunguzi siwezi kutoa maelezo zaidi ». Wakili wa mbunge Ne Mwanda Nsemi ametupilia mbali madai kwamba ni wafausi wake walioshambulia gereza kuu ya Makala,huku akiomba kueko na uchunguzi huru.

Ne Mwanda Nsemi alikamatwa kwa madai ya kumkashifu  rais Kabila kufuatia mwito alioutoiwa mwezi januari wa kutoheshimu taasisi zote za kitaifa.Wafuasi wake walikabilana na polisi mjini kati mwanzoni mwa mwezi wa machi na kusababisha watu 6 kuuliwa. Ne Mwanda Nsemi ametuhumiwa pia kuhusika na uchochezi wa chuki za kikabila.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Yusuf Saumu