1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa wa kisiasa waachiliwe huru Burma

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJL4

Umoja wa Ulaya umetoa mwito kwa utawala wa kijeshi nchini Burma,kusita kuwakamata wapinzani na vile vile wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe huru.Mawaziri wa Nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels wamesema,kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi aondoshwe kwenye kifungo cha nyumbani ili aweze kushiriki katika utaratibu wa upatanisho wa kitaifa.

Mawaziri mjini Brussels vile vile wameidhinisha vikwazo vikali dhidi ya Burma,vilivyokubaliwa na umoja huo tangu mwezi mmoja uliopita.