1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa kigeni waondoka Dubai

C.Kühntopp - (P.Martin)17 Februari 2009

Watu wamenza kuondoka Dubai.Kila siku mamia ya wageni waliopoteza ajira wanaihama Dubai.Mwenye madeni hukimbia haraka na huliacha gari lake kwenye uwanja wa ndege.Takriban kila mradi wa pili wa ujenzi umesitishwa.

https://p.dw.com/p/GwHi
The Dubai Sports City is a $4 billion, 50,000,000 square feet (4,600,000 m2) mixed-use sports city[1] currently being constructed in Dubai, United Arab Emirates. The city will consist of apartment buildings as well as several sports facilities. The first structures are due to open in late 2007. Many people believed it was going to be used in Dubai's possible bid to host the 2016 Summer Olympics, but Dubai never submitted a bid.
Uwanja wa michezo unaojengwa Dubai ukigharimu Dola bilioni 4.Picha: cc_Imre Solt_sa

Hivi sasa katika uwanja wa ndege wa Dubai makampuni ya kuondosha magari yana kazi nyingi mno.Kwani idadi ya magari yanayoachwa na wageni waliopoteza ajira na kushindwa kulipa madeni yao,inaongezeka kila siku.Hata makumpuni ya uchukuzi yanafanya biashara nzuri kwa sababu baadhi ya wafanyakazi katika sekta ya ujenzi wanapelekwa nchi zingine.

Phil Davis wa kampuni ya uchukuzi ReloGulf huko Dubai anaeleza:

"Tangu majuma mawili au matatu yaliyopita,biashara yetu imeongezeka kwa asilimia hamsini.Wengi katika sekta ya ujenzi wanakwenda Hongkong, Malaysia China au India.Wengine wanarejea nyumbani."

Nchini Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE- takriban kila mradi wa pili katika sekta ya ujenzi umekwama kwa sababu ya mzozo wa kiuchumi ulioikumba dunia nzima.Hiyo ni miradi yenye thamani ya kama Dola bilioni 582. Huko Dubai kama asilimia kumi tu ya wakaazi ni wananchi. Sehemu kubwa ya wakaazi wake ni wageni waliokwenda kufanya kazi kama vile wataalamu wa teknolojia ya mawasiliano ya intaneti kutoka Ulaya na wajenzi kutoka India na Bangladesh.

Maendeleo ya ajabu yaliyopatikana Dubai yasingewezekana bila ya wafanyakazi hao. Lakini tangu majuma kadhaa yaliyopita,wageni hao wameachishwa kazi kwa maelfu.Sheria ya nchi hiyo ya Ghuba ni wazi:Mfanyakazi anaepoteza ajira lazima aondoke nchi hiyo katika muda wa mwezi mmoja. Inatathminiwa kuwa hivi sasa,kila siku kama watu 1,500 hurejea makwao.Kwa hivyo miaka miwili ijayo,kodi za nyumba zitashuka kwa hadi asilimia 33.Kwa maoni ya Ryan Mahoney anaefanya biashara ya fenicha,mzozo huu wa fedha huenda ukatoa nafasi mpya kwa wengine. Anasema:

"Kwa miaka kadhaa tumeona makampuni na watu waliotaka kuhamia Dubai kuanzisha biashara,lakini wamehisi kuwa maisha ni ghali na hasa kodi za ofisi.Labda watu hao sasa wataitumia fursa hii na hivyo kuchangamsha upya uchumi."

Hata mkurugenzi wa kampuni ya magari ya anasa Bentley huko Dubai,Chris Buxton anaamini kuwa kipindi hiki kitapita.Anasema,Dubia ni eneo linaloinukia na hiyo humaanisha kuwa ukuaji wa uchumi utaendelea.