Wachunguzi wasikia harufu ya miili kuungua | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.06.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wachunguzi wasikia harufu ya miili kuungua

Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamesikia harufu ya kuungua kwa miili ya watu na kuona sehemu za miili imesambaa katika kijiji nchini Syria ambako mauaji makubwa yalifanyika. Watu 80, wanaripotiwa kuwa wameuwawa.

In this citizen journalism image provided by Edlib News Network ENN, anti-Syrian regime protesters chant slogans and hold a banner in Arabic that reads, Al-Qubair massacre challenges the world's humanity, during a protest against the massacre of Mazraat al-Qubair, in the northern village of Hass, in Idlib province, Syria, Thursday June 7, 2012. Syria on Thursday denied as absolutely baseless claims by opposition groups about a new massacre in the central Hama province in which government forces allegedly killed dozens of people, including women and children. (Foto:Edlib News Network ENN/AP/dapd) THE ASSOCIATED PRESS IS UNABLE TO INDEPENDENTLY VERIFY THE AUTHENTICITY, CONTENT, LOCATION OR DATE OF THIS HANDOUT PHOTO

Kijiji kilichoharibiwa cha Al-Quabair

Mahali hapo panatoa ushahidi wa uhalifu wa kutisha , amesema msemaji wa umoja wa mataifa.

Wachunguzi hao hatimaye wameweza kuingia katika kijiji hicho ambacho watu wamekimbia cha Mazraat al-Qubair baada ya kuzuiwa na majeshi ya serikali na wakaazi, na kushambuliwa kwa silaha ndogo ndogo siku ya Alhamis, siku moja baada ya mauaji hayo kuripotiwa mara ya kwanza.

Mapigano Damascus

Katikati ya jiji la Damascus , waasi walipambana na majeshi ya usalama ya serikali siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza , wamesema watu walioshuhudia , na miripuko ilisikika kwa muda wa saa kadha. Majeshi ya serikali , yamelishambulia eneo la kati la mji wa Homs mara kwa mara na majeshi hayo yalijaribu kuingia katika mji huo kutokea sehemu tatu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham Clinton amekutana na mjumbe wa kimataifa Kofi Annan mjini Washington kujadiliana nae njia ya kuokoa mpango wake unaolenga lenga wenye lengo la kusitisha umwagikaji wa damu uliodumu miezi 15 sasa nchini Syria.

Secretary of State Hillary Rodham Clinton speaks during a news conference at the State Department in Washington, Thursday, May 24, 2012, to discuss the State Department's annual report on human rights. (AP Photo/Manuel Balce Ceneta)

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham Clinton

Mataifa ya magharibi yanaulaumu utawala wa Bashar al-Assad kwa ukandamizaji wa nguvu dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali ambao ulitokana na vuguvugu la maandamano ya umma katika mataifa ya Kiarabu.

Kikosi cha umoja wa mataifa cha waangalizi ni kundi la kwanza huru kuwasili katika kijiji cha Mazraat al-Qubair, kijiji ambacho kilikuwa kinaishi watu wapatao 160 katikati ya jimbo la Hama. Wanaharakati wa upinzani na maafisa wa serikali ya Syria wanalaumiana kwa mauaji hayo na kutofautiana juu ya idadi ya watu waliouwawa.

Taarifa zatofautiana

Wanaharakati wanasema kuwa watu zaidi ya 78, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto wamepigwa risasi, kukatwakatwa na kuchomwa moto hadi kufa, wakisema wanamgambo wanaounga mkono serikali wanaojulikana kama Shabiha, wanahusika na mauaji hayo.

Taarifa ya serikali kupitia shirika la habari la nchi hiyo SANA , imesema kuwa makundi ya magaidi wenye silaha yamewauwa watu tisa wanawake na watoto kabla ya maafisa wa Hama kuitwa na kuwauwawa washambuliaji hao.

Ssusan Ghosheh , msemaji wa kundi la wachunguzi wa umoja wa mataifa, amesema idadi ya watu waliouwawa inayotolewa na wakaazi inapingana na kwamba wanahitaji kufanya uchunguzi wao binafsi wa majina ya watu ambao hawajulikani waliko na watu waliouwawa kwa kulinganisha na orodha inayotolewa na wanakijiji wa kijiji cha karibu.

Harufu ya kuchomwa watu

Unaweza kusikia harufu ya miili ya watu iliyoungua , Ghosheh amesema. Unaweza pia kuona sehemu za miili katika kijiji hicho, ameongeza Ghosheh.

epa03253043 A staffer of a hotel lift the national flag next to UN cars parked behind him, in Damascus, Syria, 07 June 2012. According to media reports on 07 June 2012, the Syrian army and civilians prevented UN observers from inspecting the site of a reported massacre in the central province of Hama, the head of the UN mission in the country confirmed. EPA/YOUSSEF BADAWI

Wachunguzi wa umoja wa mataifa nchini Syria

Ujumbe wa uchunguzi wa umoja wa mataifa umetoa taarifa siku ya Ijumaa ikisema kuwa alama za magurudumu ya magari yenye silaha ilikuwa inaonekana wazi katika eneo hilo na baadhi ya nyumba zimeharibiwa kwa makombora na maguruneti. Ndani baadhi ya nyumba , damu ilikuwa inaonekana katika kuta na sakafu, taarifa hiyo imesema.

Wakati huo huo , kiasi watu 12, ikiwa ni pamoja na wanawake wanane , wameuwawa na jeshi la Syria katika mji wa kusini wa Deraa usiku wa Ijumaa, limesema kundi la wanaharakati wanaoangalia hali ya haki za binadamu nchini Syria.

Mwandishi: Sekione Kitojo /afpe/ape

Mhariri: Bruce Amani

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com