1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mishahara ya wabunge

Mtullya, Abdu Said21 Mei 2008

Wabunge wa Ujerumani wakataa pendekezo juu ya kuongezewa mishahara .

https://p.dw.com/p/E3w7
Wabunge wa Ujerumani wapinga mpango wa kuongezwa mishahara.Picha: picture-alliance/ dpa


Wabunge  wa Ujerumani  wamekataa pendekezo  ambalo lingewezesha mishahara yao kuongezwa kwa  asilimia 16 nukta 4 .

Pendekezo hilo pia lilipingwa vikali na vyama vya upinzani pamoja na wananchi.

Pendekezo la  kuongeza  mishahara ya wabunge 612  hapo  awali  pia  liliungwa mkono  na kansela wa  Ujerumani Angela Merkel aliesema kuwa lengo lilikuwa kusawazisha mishahara ya wabunge na ya mahakimu.

Lakini ,kwa mujibu wa vyombo  vya habari kansela Merkel  na baraza lake la mawaziri pia wapo tayari kusamehe nyongeza za mishahara yao.

Msemaji  wa serikali ya Ujerumani ameeleza kuwa  Kansela Merkel alitangaza  uamuzi huo  mapema leo kwenye baraza lake  la  mawaziri. 

Kutokana na  malalamiko  makubwa ya wananchi viongozi wa vyama vya CDU na SDP vinavyoongoza serikali ya Ujerumani waliamua jana kusimamisha mpango juu ya kuongeza mishahara ya wabunge wa vyama  vyao.

Mishahara hiyo  ingelifikia  Euro 7,946 kwa mwezi.