1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge Tanzania wahofia maisha yao

Mohammed Khelef25 Novemba 2014

Wabunge wanaounga mkono kuwasilishwa na kujadiliwa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali nchini Tanzania juu ya kashfa ya Tegeta Escrow Account wanaripoti kutishiwa maisha yao siku moja kabla ya ripoti hiyo.

https://p.dw.com/p/1DsdO
Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Sospeter Muhongo, ambaye wizara yake inasimamia Shirika la Umeme, TANESCO.
Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Sospeter Muhongo, ambaye wizara yake inasimamia Shirika la Umeme, TANESCO.Picha: DW/J. Hahn

Hali kwenye mji mkuu wa Tanzania, Dodoma, ambako ndiko vinakoendelea sasa vikao vya bunge hilo inatajwa kuwa tete, chini ya masaa 24 kabla ya kuwasilishwa ripoti ya uchunguzi juu ya kashfa hiyo inayotajwa kuwa moja ya kashfa kubwa kabisa kuwahi kulikumba taifa hilo la Afrika ya Mashariki ikiwahusisha vigogo na wafanyabiashara kadhaa.

Mohammed Khelef alizungumza na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ndiye kwa mara ya kwanza aliyeiibua kashfa hiyo bungeni na ambaye, pamoja na wabunge wengine kadhaa wanaopigania kuwajibishwa kwa wahusika, analalamikia kutishiwa usalama wa maisha yao.

Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi