1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa shambulia Niger Delta

19 Septemba 2008

Waasi katika eneo la Ogoni huko Nigeria wadai wameshambulia zana za kampuni la mafuta la Shell.

https://p.dw.com/p/FLTJ

Kikundi cha wafuasi wenye siasa kali huko Niger delta,kusini mwa Nigeria-The Movement for the Emancipation of the Niger delta- kimearifu kimeteketeza bomba kubwa la mafuta mali ya kampuni la Royal Dutch Shell.Hakujakuwa na taarifa ya haraka kutoka kwa kampuni la Shell.

Taarifa nyengine ilisema kuwa juhudi za amani katika eneo la Ogoni , hazitafanikiwa ikiwa serikali ya Nigeria itaendelea kukataa kushauriana na wenyeji kuhusu shughuli za uchimbaji mafuta.Wenyeji wa Ogini wanadai mazingira yao yanachafuliwa na wao hawafaidiki na biashara ya mafuta yao.

Hujuma hiyo ni ya 5 katika zana za kampuni la Shell huko River State -kitovu cha shughuli za uchimbaji mafuta nchini Nigeria.Kikundi hicho chenye siasa kali kimetishia kutanua hujuma zake hadi mikoa mingine inayozalisha mafuta nchini Nigeria mfano Bayelsa na Delta pamoja na kuhujumu hata visima 2 vya mafuta vya baharini - Bonga na Abgami-cha kwanza ni cha shell na cha pili cha kampuni la Chevron.

Ni Juni mwaka huu, pale kikundi hicho cha MEND kilipofanya shambulio katika kisima cha Bonga - ambacho hadi wakati huo kikifikiriwa ni cha usalama kabisa na vigumu kukifikia.

Tangu kuchomoza kwa kikundi hiki hapo 2006, kudai sehemu kubwa ya pato la mafuta kutoka visima vya kusini mwa Nigeria itumike kwa manufaa ya wakaazi wake, kimepunguza pato la mafuta kutoka Nigeria kwa kiasi cha robo moja.

MEND iliarifu mapema jana kuwa wapiganaji wake usiku wa manane waliwakabidhi mahabusu 2 wa Afrika kusini mikononi mwa askari kanzu. Walidai waliwaokoa mikononi mwa maharamia. Baadae ilipangwa wakabidhiwe Ubalozi wa Afrika kusini mjini Port Hercourt.

Utaratibu wa kusaka amani katika eneo la Ogoni-mtihani mkubwa katika kuleta hali ya utulivu Niger delta,eneo nono kwa mafuta,yamkini usifanikiwe ikiwa serikali ya Nigeria itakataa kushauriana na jamii za wenyeji kuhusu uchimbaji wa mafuta katika maemneo yao.

Uamuzi wa serikali ya Nigeria wa Juni,mwaka huu kuondoa shughuli za uchimbaji mafuta za kampuni la Shell katika ardhi ya ogoni, ulishangiriwa awali kama ni ushindi wa juhudi zisizotumia nguvu dhidi ya kampuni la kimataifa.Haukupita muda lakini, serikali ya Nigeria ilisema nafasi ya Shell itachukuliwa na na kampuni la kinigeria la uchimbaji mafuta-Nigerian Petrolium Developement Company.Waogoni wanahisi uamuzi huo wa serikali ya Nigeria bila kuwashauri wao ni jaribio jengine la kuwanyima sehemu yao katika biashara ya mafuta.

Kikundi cha kimataifa kinachojishughulisha na msukosuko wa Ogoni, kimependekeza serikali ya shirikisho la Nigeria ishike usukani kuongoza mapatano ya pande tatu ikiingiza makampuni ya mafuta na waakilishi wa Ogoni juu ya masharti ambayo yanapaswa kutimizwa kabla ya uchimbaji mafuta.

Isitoshe imegunduliwa kwamba hakuna mengi yaliofanywa kusafisha mazingira yaliochafuliwa na miongo 3 ya makampuni ya mafuta.Wala wakaazi wa Ogoni hawakulipwa fidia. Rais Umaru YarźAdua wa Nigeria amedai kwamba mapatano yamefikiwa juu ya ulipaji fidia.Viongozi wa Ogoni lakini ,wanasema swali la fidia halikuzungumzwa.Mpango wa kuyasaifisha mazingira yao na Shirika la Mpango wa kimazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) umekwama.

Serikali ya Nigeria kwhaivyo, imetakiwa kuhrakisha usafishaji wa mazingira na malipo ya fidia kwa jamii zilizoathirika na uchafuzi wa mazingira . Pia ishughulikie maswali makubwa zaidi yanayohusu ukosefu wa maendeleo ya kiuchumi ya wakaazi wa Niger Delta.