1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Libya ziarani Marekani

Halima Nyanza14 Mei 2011

Marekani imeliita Baraza la Mpito la taifa la waasi wa Libya kuwa ni kundi la ''wapatanishi halali''.

https://p.dw.com/p/11FyF
Kiongozi wa Libya Moammar GaddafiPicha: dapd

Marekani hata hivyo, haikulipa kundi hilo hadhi ya kulitambua kidiplomasia baada ya mkutano na waasi hao wa NTC katika Ikulu ya Marekani jana. Waasi hao, wakiongozwa na kiongozi wao Mahmud Jibril wako mjini Washington Marekani kushinikiza kutambuliwa rasmi na kupata misaada zaidi ya kifedha.

Wakati huohuo, televisheni ya taifa ya Libya  ilirusha taarifa anayoripotiwa kuwa ni ya kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, ambaye alikuwa akilaani shambulio la Alhamisi lililofanywa na majeshi ya NATO katika makaazi yake. Licha ya ripoti zilizotolewa awali kwamba kiongozi huyo wa Libya amejeruhiwa katika shambulio hilo, amesema katika taarifa yake kwamba hakudhurika na yuko katika sehemu ambapo mabomu ya majeshi ya NATO hayawezi kumfikia. Msemaji wa Gaddafi amesema kiongozi huyo bado yuko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.

Tripolis NATO Luftangriff Gaddafi
Shambulio lililofanywa na jeshi la NATO, katika makaazi ya GaddafiPicha: picture-alliance/dpa