1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa kimaksi bado wanawazuilia mateka

31 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CiNm

Waasi wa kimaksi nchini Colombia bado wanawazuilia mateka watatu wanaosubiri kuachiwa huru hii leo.

Rais wa Venezuela, Hugo Chavez, ameelezea wasiwasi wake kwamba hatua hiyo huenda ikahatarisha kuachiwa huru kwa mateka hao kufuatia makubaliano aliyoyafikia pamoja na waasi hao wa kimaksi.

Kuachiwa kwa wanasiasa wa Colombia na mtoto aliyezaliwa na mmoja wa mateka hao, kulikuwa kumepangwa kufanyike Alhamisi iliyopita, lakini kumekuwa kukiahirishwa siku baada ya siku kwa kuwa waasi wamekataa kusema mahala walipo.

Mapema mwezi huu kundi hilo lilitangaza kuwa litawakabidhi mateka hao kwa rais Hugo Chavez au mjumbe atakayetumwa na kiongozi huyo.