1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Waasi wa Chad wauvamia mji wa Adre karibu na Darfur

Waasi bado wanakabiliana na wanajeshi wa serikali mjini Ndjamena

default

Wanajeshi wa Ufaransa mjini Ndjamena wakiwahamisha raia wa kigeni kutoka Chad

Waasi nchini Chad ambao inasemekana wamesaidiwa na ndege za jeshi la Sudan, wamefanya shambulio hii leo katika mji wa Adre mashariki mwa Chad, unaopakana na jimbo la Darfur.

Afisa mkuu wa serikali ya mtaa mjini humo, Abadi Sasir, amethibitisha shambulio hilo akisema idadi kubwa ya waasi wameingia mjini humo lakini wanakabiliana nao.

Kwa mujibu wa afisa huyo waasi wa Chad wamesaidiwa na helikopta na ndege aina ya Antononov za Sudan. Waasi na majeshi ya serikali yanakabiliana katika mapambano ya kuudhibiti mji mkuu Ndjamena. Afisa wa serikali ya Chad amesema jeshi la nchi hiyo linaudhibiti mji wa Ndjamena.

Leo wizara ya mashauri ya kigeni ya Ufaransa imesema imewaondoa raia 514 wa kigeni kutoka Chad na kuwasafirisha hadi mjini Libreville nchini Gabon, wakiwemo wafaransa 217.

Taarifa ya wizara hiyo imesema raia wengine takriban 400 wa kigeni waliosalia mjini Ndjamena wataondolewa baadaye.

Ufaransa inapanga kuwasafirisha raia wake kutoka mjini Libreville hadi Paris hii leo.

Wakati haya ya kiarifiwa Nigeria imeliweka jeshi lake katika hali ya tahadhari huku kukiwa na hofu ya mapigano nchini Chad kuenea.

 • Tarehe 14.02.2008
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D1la
 • Tarehe 14.02.2008
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D1la

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com