1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi Libya wasogea Sirte

30 Agosti 2011

Waasi Libya wasema huenda wamemuua Khamis Gaddafi na mkuu wa upelelezi Abdullah al Senussi

https://p.dw.com/p/12Pia
Waasi Libya waendelea na mapambanoPicha: dapd

Maafisa wa uasi nchini Libya wamesema wanaelekea kuwa na uhakika kuwa wamemuua mkuu wa upelelezi wa kiongozi wa nchi hiyo, Muammer Gaddafi, Abdullah al Senussi, pamoja na mojawapo ya wanawe wa kiume wa kiongozi huyo, Khamis Gaddafi.

Libyen Chamis Gaddafi Sohn von Muammar Gaddafi getötet
Mwanawe wa kiume wa mwisho Muammer Gaddafi, Khamis GaddafiPicha: PA/abaca

Khamis ni mwanawe wa mwisho wa Gaddafi, na kifo chake kimetangazwa mara kadhaa tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mapema mwaka huu.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Algeria, amesema mkewe Gaddafi na wanawe watatu wamewasili Algeria hapo jana asubuhi. Nchini Libya, Shirika la kujihami la NATO linaendelea kufanya mashambulio ya angani dhidi ya vituo vya jeshi mjini Sirte, katika kuusaidia uasi kusogea mjini humo.

Sirte ni mji alikozaliwa Gaddafi, ambako fununu zimeenea kuwa huenda akawa amejificha huko.

Mwandishi Maryam Abdalla/rtre, afpe, dpae
Mhariri: Aboubakary Liongo