1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi 10 wa Tamil Tigers wameuwawa

31 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CiWT

Jeshi la anga la Sri Lanka limeishambulia kwa mabomu kambi ya waasi wa Tamil Tigers kaskazini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi amesema wanajeshi wa jeshi la ardhini wamewapiga risasi na kuwaua waasi wasiopungua 10 katika matukio matatu tofauti.

Shambulizi la angani limefanywa leo huko Muthiyankattu katika wilaya ya Mullaitivu, yapata kilomita 380 kaskazini mashariki mwa mji mkuu, Colombo.

Marubani wa jeshi wamesema wamefaulu kuilenga kambi ya waasi wa Tamil Tigers.