1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wa DW wanyang'anywa vidio Uturuki

7 Septemba 2016

Zaidi ya waandishi habari 100 wa Ujerumani wameazimia kuiwekea mbinyo serikali ya Uturuki kuhusiana na ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari baada ya jaribio la mapinduzi.

https://p.dw.com/p/1JwrQ
DW Conflict Zone Türkei - Gast Akif Çağatay Kılıç
Waziri wa vijana na michezo wa Uturuki Akif Cagatay Kilic(kulia)Picha: DW/M. Martin

Mashirika makubwa yanayotetea uhuru wa vyombo vya habari yameanzisha ombi mwezi Augusti linaloitaka serikali ya Ujerumani na halmashauri ya Umoja wa Ulaya kuweka msimamo wa wazi kuhusu suala hilo.

Tarehe 5 Septemba , waandishi habari wa Deutsche Welle walinyang'anywa picha ya vidio na maafisa wa serikali ya Uturuki kufuatia mahojiano ya televisheni na waziri wa vijana na michezo wa nchi hiyo Akif Cagatay Kilic. Mwandishi anayehusika na kipindi cha maeneo ya mizozo "Conflict Zone" cha televisheni ya DW Michael Friedmann alielezea kwamba:

"Nafikiri waziri hakupendezwa na mahojiano hayo. Maswali hayakuwa yale aliyoyakubali na kutarajia na kwa hiyo , na huu ni ushahidi hali ni mbaya kiasi gani kwa utawala wa kidemokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini Uturuki, alikuwa anaonekana kuwa na mamlaka kupita kiasi.

DW Conflict Zone Türkei
Mtangazaji wa kipindi cha "Conflict Zone" cha DW Michel FriedmannPicha: DW/M. Martin

Baadaye afisa wa habari wa waziri huyo alihalalisha tukio hilo kwa kudai kwamba maswali aliyoulizwa wakati wa mahojiano hayakuwa yale yaliyoidhinishwa na serikali kabla.

Mahojiano hayo yaliyosababisha utata yaliongozwa na mtangazaji wa kipindi hicho Michel Friedmann mjini Ankara siku ya Juamtatu jioni. Friedmann alimuuliza waziri huyo wa vijana na michezo, Akif Cagatay Kilic juu ya jaribio la mapinduzi mwezi Julai pamoja na kuwasimamisha kazi mamia kwa maelfu ya watu pamoja na kukamatwa ambako kulitokea baada ya jaribio hilo.

Mwandishi: Sekione Kitojo/DW English

Mhariri: Caro Robi