1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi habari 86 wauwawa 2007

3 Januari 2008

Mwaka 2007 ulikuwa mwaka wa maafa kwa waandishi habari ulimwenguni na habari zikichujwa baadhi ya nchi.

https://p.dw.com/p/CjoM

Jumuiya ya waandishi habari ulimwenguni iitwayo „RIPOTA BILA MIPAKA“ ilitoa jana ripoti yake ya mwaka huko Berlin, ikisimulia idadi ya waandishi habari waliouwawa wakifanya kazi zao za uenezaji habari na wale waliotiwa korokoroni ingawa „mjumbe hauwawi“.

Visa na mikasa iliowafika waandishi habari mwaka 2007 sio tu vinahuzunisha bali hata vinavunja moyo.Kwamuujibu wa ripoti ya Jumuiya hii jumla ya waa ndishi habari 86 waliuwawa kutokana au wakati wa shughuli zao za uwandishi-habari:

Iwapo ni nchini Irak,Somalia,China au visiwani Kuba, waandishi habari wanaishi hatarini.Wanajikuta kati kati ya safu za mapigamno ya vita vya kienyeji kama hali ilivyo wakati huu nchini Kenya au wanahatarika kwavile wanawakera watawala kwa kufichua ukweli wa hali ya mambo.

Kwa muujibu wa Jumuiya hii ya maripota wasio na mpaka, katika visa 90% vya waandishi-habari waliouwawa wale waliohusika na vifo vyao hawakushtakiwa wala kuadhibiwa.

Hii ni hali ya kusikitisha kwa jicho kuwa mwaka uliopita wa 2007 rekodi ilifikiwa ya vosa vya kusikitisha vya maafa yaliowafika waandishi habari.

Si chini ya waandishi habari 86 wamepoteza maisha yao wakati wakifanya kazi yao.Hii ni idadi kubwa kabisa tangu 1994-imearifu jumuiya ya maripota wasio na mipaka hiyo jana mjini Berlin.

Kwa mara ya 5 mfululizoIrak mwaka jana wa 2007 imekuwa ndio nchi hatari kabisa kwa waandishi habari kwa muujibu anavyoelezea Katrin Evers,msemaji wa jumuiya ya waandishi habari wasio na mipaka:

„mwaka 2007 uliopita ,“Jumuiya ya waandishi habari bila mpaka“, imejionea tena nchini Irak idadi kubwa kabisa ya waandishi habari waliouwawa wakifanya kazi zao.Irak waliuliwa waandishi 47 na kwahivyo, kwa mara nyengine tena imeibuka kuwa nchi hatari kabisa kwa waandishi habari ulimwenguni.Irak, inafuatiwa na Somalia .Nchini Somalia waandishi-habari 8 waliuliwa.Nchini Pakistna ni 6 wakati kisiwani Sri Lanka,wtatu walianguka mateka.“

Katika waandishi habari waliouwawa nchini Irak ni pamoja na mrusi na muiraki.Waandishi habari zaidi waliouwawa ilikuwa nchini Eritrea,Afghanistan,kisiwani haiti,nchini Mexico,Nepal lakini pia Uturuki na hata Marekani.Kwa jumla katika nchi 21 wasandishi habari wamepoteza maisha yao mwaka uliopita.

Kwa hivyo, anasema Bibi Evers wa jumuiya hiii ya waandishi habari mwaka uliomalizika wa 2007 ndio mwaka uliojionea kuuwawa kwa waandishi wengi kabisa tangu 1994.

Hata idadi ya waandishi waliotekwanya pia ilikuwa kubwa 2007.

Jumla ya waandishi habari 67 walitekwanyara katika jumla ya nchi 15 mbali mbali.Mwaka mpya wa 2008 ulipoingia kiasi cha waandishi habari 135 walikuwa bado gerezani na 887 walitiwa nguvuni mwaka jana pekee.Gereza kubwa kwa waandishi habari linakutikana China na Kuba.

Hata katika nchi kama Burma ,Syria na Iran habari zinachujwa wakati katika nchi nyengine vyombo vya habari vya serikali ndio sauti pekee kwa umma.Mtandao wa Internet kwa kadiri kubwa unakaguliwa .

Uhuru wa waandishi habari na uenezaji habari na hasa ule wa kukereketa hauheshimiwi katika nchi nyingi ulimwenguni na waandishi habari wanaochimba kinapita nini chini kwa chini na kukiripoti,wanaishi hatarini.