1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wakusanyika Thailand

Admin.WagnerD3 Februari 2014

Wapinzani nchini Thailand wameanza kukusanyika kwa ajili ya kufanya maandamano makubwa katikati ya jiji la Bangkok, yenye lengo la kusukuma mbele jitihada zao za kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Jumatatu.(03.02.2014)

https://p.dw.com/p/1B1pX
Thailand Protest Demonstranten Anti Regierung Wahl 3.2.14
Waandamanaji wakiwa wamekusanyika mjini Bangkok nchini ThailandPicha: Reuters

Waandamanaji hao wanaoipinga serikali wamejenga mahema na kuweka kambi yao kaskazini mwa mwa jiji la Bangkok ikiwa ni jitihada ya kuongeza mbinyo zaidi kwa serikali ya taifa hilo ijiuzulu. Baadhi yao wamejiunga na kiongozi wa maandamano Suthep Thaugsuban kutembea kwa miguu na wengine wakiwa katika magari ikiwa siku moja baada ya uchaguzi uliogubikwa na vurugu.

Wengine wamelizingira jengo lenye ofisi za serikali huko kaskazini mwa Bangkok, jengo ambalo inaelezwa Waziri Mkuu Yungluck na mawaziri wawili waandamizi wanafanya mkutano wao na kwamba waandamaji hao walikata waya wa umeme ulizunguka jengo hilo. Lakini hawajaingia ndani na wala haijawa wazi kama Yingluck bado yupo katika jengo hilo.

Harakati za waandamanaji

Pamoja na kuwepo kwa wasiwasi wa kutoka vurugu, mchakato wa upigaji kura uliendelea kwa amani katika asilimia 90 ya vituo vya kupigia kura nchini humo hapo jana. Waandamanaji walilazimisha vituo vya kupiga kura vilivyopo karibu mji wa Bangkok na upande wa kusini wa Thailand vifungwe.

Thailand Protest Demonstranten Anti Regierung Wahl 3.2.14
Waandamanaji wanaopinga serikali ThailandPicha: Reuters

Hatua hiyo inaelezwa kuwanyima haki ya kupiga kura mamilioni ya raia wa taifa hilo na kusababisha baadhi ya nafasi ya wabunge kutojazwa na kutoa fursa ya kufanyika uchaguzi mwingine mdogo kwa lengo la kusawazisha kasoro hizo. Duru zinaeleza hali hiyo itachangia pia mkwamo wa kiasiasa kwa miezi kadhaa.

Chama cha Upinzani nchini Thailand ambacho kinaunga mkono waandamanaji na kiligomea uchaguzi huo, kimesema kinajiridhisha kwa kuangalia vifungu vya wa kisheria katika uchaguzi huo ili kuweza kubatilisha uchaguzi huo.

Jitihada za kusimamisha uchaguzi, ni seheme ya mgogoro wa takribani miezi mitatu ambao umeligawanya taifa hilo kati ya wanaomuunga mkono Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra na upinzani ambao unautuhumu utawala wake kwa kukithili kwa rushwa. Maandamano yalitanda katika maeneo muhimu mjini Bangkok na kulazimisha baadhi ya wizara kusimamisha majukumu yao katika ofisi zilizopo katika maeneo hayo na kutafuta maeneo mengine ya kufanyia kazi.

Kiongozi wa waandamanaji Suthep Thaugsuban alisikika akisema " Hatuwezi kusitisha mapambano. Tutaendelea na mapmabano kupambana. dhamira yetu kufanya serikali ijiuzulu kwa hivyo msitutake kuachana na harakati hizo" alisema kiongozi huyo.

Suthep mwenye haiba ya uzungumzaji na mbunge wa zamani amewataka waandamanaji kujitokeza kwa wingi katika maeneo tofauti ya kibiashara, pamoja na Bankok na miji mininge pia.

Waandamanji hao wanataka kuondoshwa utawala uliopo na kuwepo kwa baraza la maalumu ambalo litakuwa na majukumu ya kuandika upya katiba na sheria za uchaguzi kwa lengo ka kukabiliana na vitendo vya rushwa katika chaguzi. Waziri Mkuu Yingluck amekataa kujiuzulu kwa kusema amechaguliwa kwa kishindo na kwamba pia yupo tayari kwa mageuzi na kwamba kuundwa kwa baraza hillo kutakuwa kinyume cha katiba na si suala la kidemokrasia.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR/APE
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman