1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita juu ya vyakula?

Dreyer, Maja14 Aprili 2008

Wahiri wa magazeti ya Ujerumani wanazingatiwa kupanda kwa bei za vyakula na athari zake.

https://p.dw.com/p/DhNK
Bei za mahindi zimepanda pamoja na za vyakula vinginePicha: AP


Kwanza ni gazeti la “Frankfurter Rundschau” ambalo linauliza hivi:


“Je, katika karne hii ya 21. kutakuwa na vita vya kupigania mkate, mchele na chapati? Kwa sasa, fedha za kuzuia janga zitapatikana, lakini kwa njia hiyo hali haitaboreshwa, bali ni kazi itakayochukua muda mrefu kujenga sekta ya kilimo katika nchi zinazoendelea ambayo haitegemei bidhaa za kutoka nje. Kwani msaada wa maana kwa ukulima wa nchi maskini unamaanisha kupunguza ruzuku kwa wakulima wa kienyeji katika nchi tajiri na hivyo kukubali kuacha kupata faida kwenye soko la kimataifa ambalo hadi sasa si huru.”


Moja kwa moja tuendelee na gazeti la “Leipziger Volkszeitung”. Limeandika:

“Soko halina dhamira. Na kwa bahati mbaya, hata wanasiasa wanaohusishwa na ukulima pia hawana dhamira, kwani wangekuwa nayo, basi wangekuwa wameshafuta ruzuku kwa wakulima wa nchi tajari ambazo zinalinda soko la kienyeji dhidi ya bidhaa rahisi kutoka nchi zinazoendelea. Basi, muda umewadia kuweka huru soko la vyakula. Na pia inabidi kuwa na msaada wa maendeleo unaolenga nchi maskini ziongeze kuzalisha vyakula ili ziweze kunufaika kutokana na bei kupanda.”


Sababu moja ya bei za vyakula kupanda haraka katika miaka iliyopita inasemekana kuwa uzalishaji wa mimea kwa ajili ya kutengeneza mafuta ya magari. Mhariri wa “Rhein-Zeitung” pia ana wasiwasi akiandika:


“Wataalamu wachache walikuwa na mashaka kutumia vyakula kama mafuta tangu mwanzoni. Lakini baada ya muda watu wengi wamefahamu hasara yake. Basi tufanyaje? Kwanza inabidi tufahamu kwamba ulimwengu wetu hauwezi kutumiwa bila ya kikomo. Matokeo yake yanaweza kuwa kwamba mkate unafaa kuwekwa mezani badala ya kutiwa kwenye bomba la mafuta.”