1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Virusi vya Zika havitaathiri michezo ya Olimpiki

29 Januari 2016

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki – IOC itatoa mwongozo wiki hii unaolenga kuwakinga wanariadha na wageni dhidi ya Zika, virusi vinavyosababishwa na mbu ambavyo vinasambaa kwa kasi kote Amerika ya Kusini

https://p.dw.com/p/1Hlz0
Brasilien Recife Anti Zika Virus Einsatz Mücken Besprühung
Picha: Getty Images/AFP/C. Simon

Hayo yanajíri ikiwa ni miezi michache tu kabla ya kuanza Mashindano ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro mwezi Agosti.

Rais wa IOC Thomas Bach amesema arifa itatumwa kwa Kamati za Kitaifa za Olimpiki, wakati mji wa Rio ukijiandaa kuandaa tamasha kubwa kabisa la michezo kuwahi kuandaliwa katika ardhi ya Amerika Kusini kwa mara ya kwanza.

Wizara ya michezo ya Brazil imeema kuwa ungonjwa wa Zika hautaiathiri michezo hiyo ya msimu wa joto. Waziri wa michezo George Hilton amesema mipango maalum imewekwa ili kuhakikisha kuwa maeneo ya michezo ni safi kuanzia mwanzoni mwa mashindano hadi mwisho. "kwa sasa tunashirikiana na wizara zote na kamati zote za serikali, serikali zote za majimbo na mitaa, na umma ili kumaliza kazi hii ngumu. Idara za uangalizi za Olimpiki, makundi ya ukaguzi wa matibabu, na watalaamu wa matibabu wanafanya kazi kutengeneza chanjo. Tunafanya mengi katika kuzuia virusi hivyo".

Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO limeonya kuwa ugonjwa huo, unaohusishwa na ulemavu wa maelfu ya watoto waliozaliwa, unasambaa kwa kasi na unaweza kuwaathiri hadi watu milioni nne katika bara la Amerika Kusini.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Daniel Gakuba