1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIRGINIA:Sudan yaamriwa na mahakama kulipa fidia ya dola millioni 8

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfH

Mahakama moja nchini Marekani imeiamuru Serikali ya Sudan kulipa fidia ya dola milioni 8 kwa familia za askari 17 wa jeshi la majini la Marekani waliyouawa katika shambulio la kujitoa mhanga nchini Yemen mwaka 2000.

Jaji wa mahakama hiyo Robert Doumar amesema kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa Sudan iliwasaidia magaidi wa kundi Al Qaida wanaotuhumiwa kwa shambulio hilo.

Sudan imekuwa ikikanusha kuhusika na kundi hilo la Al qaida na imeshindwa katika majaribio kadhaa ya kutaka kufutwa kwa kesi hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na familia za wahanga wa tukio hilo ambao walikuwa wakitaka fidia ya dola milioni 105 kutoka serikali ya Sudan.

Katika shambulio hilo la mwaka 2000 wanamaji 17 wa Marekani waliuawa na wengine 39 kujeruhiwa baada ya washambuliaji wakiwa katika boti iliyojaa milipuko walipojibamiza kwenye meli ya kivita ya Marekani kwenye ufuko wa Yemen.