1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa nchi za eneo la euro wakutana

23 Oktoba 2011

Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya wameidhinisha masharti magumu kuhusiana na mitaji kwa ajili ya mabenki kupata mitaji. Baada ya mkutano wa takribani saa 10 uliofanyika jana mjini Brussels.

https://p.dw.com/p/12x8i
Kansela Angela Merkel na Rais Nicolas Sarkozy wa UfaransaPicha: dapd

Mawaziri hao wamekubaliana kuingiza kiasi cha euro bilioni100 katika mabenk ya ulaya, nyingi za hizo huenda zikaathirika kutokana na kununua dhamana zisizolipika za serikali ya Ugiriki. Ureno, Italia na Uhispania zimepinga mpango huo kutokana na ughali wake ikilinganishwa na uwezo wao. Lakini shinikizo kutoka kwa nchi 24 za umoja wa Ulaya limezishawishi zikubaliane na mpango huo. Mawaziri hao wa fedha watawasilisha mpango kwa ajili ya viongozi wa serikali unaotarajiwa kufanyika leo. Katika mkutano huo viongozi hao wanatarajiwa kupiga hatua ya namna ya kutumia mfuko wa uokozi wa eneo la euro wenye thamani ya euro bilioni 440.