1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G20 Wakutana.

Sudi Mnete/Reuters13 Machi 2009

Mawaziri wa Fedha na Wakuu wa Mabenki kutoka nchi zilizoendelea kiviwanda Duniana G20 wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo nchi Uingereza kujadiliana namna ya kutatua mgogoro wa Kiuchumi unaoukumba Dunia.

https://p.dw.com/p/HBFg
Baadhi ya viongozi wanaohudhuria mkutano wa nchi zilizoendelea kiviwanda -G20- unaofanyika London, Uingereza.Picha: AP

Mkutano huo unafanyika kabla ya mkutano wa Kilele wa Viongozi Wakuu wa nchi hizo za G20 utakaofanyika tarehe pili mwezi aprili.

Mkutano huo wenye lengo la kuwapa mwelekeo wa kutoa maamuzi viongozi wakuu wa nchi za G20 unafanyika kukiwa na changamoto ya mataifa hayo kutekeleza mipango iliyopo katika kunusuru uchumi wa nchi zao pamoja na kuibua mikakati mipya.


Miongoni mwa mambo yatakayotazamwa kwa kina katika Mkutano huo ni namna ya kila nchi ilivoshiriki kuukabili mgogoro wa kiuchumi na vikwazo vyake baada ya maazimio ya mkutano wa mataifa hayo yaliyofikwa mwezi Novemba mwaka jana.


Mkutano wa G20 wa Aprili unatajwa kuwa na wa mvutano mkali baada ya Marekani kutaka mataifa hayo yatenge asilimia mbili ya pato lake kuchechea matumizi ili kuinua uchumi jambo ambalo limepingwa vikali na nchi za Ufaransa na Ujerumani.


Mataifa mengine kama Japan na China leo yameongezea bajeti matumizi ya Serikali zake kwa lengo la kukabiliana na tatizo la mgogoro wa kiuchumi


Waziri wa Fedha wa Japan, Kaoru Yosano, amesema nchi yake imeitikia mwito wa kuinua uchumi wake na kuahidi kufanya jitihada zaidi katika kunusuru uchumi huku China nayo ikisema itafanya jitihada nyingine zaidi kukabiliana na hali hiyo.


Naye Waziri Mkuu wa China ameyataka mataifa hayo yaliyo katika G20 kutoa kipaumbele kwa mataifa yanayoendelea katika kujaidili namna ya kuyanusuru na kasi ya mgogoro huo wa Kiuchumi inayoendelea hivi sasa


Waziri Mkuu Jiabao amesema Mataifa hayo lazima yaendelee kusaidia katika kufikia Malengo ya Milenia pamoja na Uboreshaji wa Kisera ili kuupiga vita umasikini na kupunguza athari za Mgogoro wa Kiuchumi.


Mgogoro wa uchumi ambao umeikumba Dunia umeathiria nchi nyingi Duniani na umeacha idadi kubwa ya watu bila ajira na kwa mujibu wa IMF hali hiyo inaweza kuwa mbaya zaidi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.