1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vyaongezeka zaidi nchini Norway

23 Julai 2011

Polisi nchini Norway imesema kuwa kiasi watu 80 wameuwawa katika shambulio katika kambi ya vijana ya chama tawala cha Labour karibu na mji mkuu Oslo na wakiwemo kumi katika shambulio la Bomu.

https://p.dw.com/p/12271
Waziri Mkuu wa Norway Jens StoltenbergPicha: AP

Akizungumza katika hotuba kwa taifa hilo Waziri Mkuu wa Norway, Jens Stoltenberg, ametoa wito kwa wananchi kusimama pamoja baada ya kutokea mashambulizi mawili tofauti nchini humo.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari jana usiku ,Stoltenberg amesema Norway inapaswa kujibu shambulio hilo kwa demokrasia zaidi na uwazi bila ya wasiwasi wowote.

Kiasi ya watu saba waliuwawa jana mchana baada ya kulipuka kwa bomu katikati ya mji wa Oslo. Shambulio hilo lilisababisha kuvunjika kwa jengo ambalo ni ofisi ya waziri mkuu.

Kufuatia tukio hilo Rais Barack Obama wa Marekani ametuma salamu za rambi raambi."Kwa sasa hatuna taarifa, lakini binafsi nataka kutoa pole yangu kwa watu wa Norway na kwamba kisa hicho kinatukumbusha jumuya ya kimataifa, kushikamana kuzuia matukio haya ya kigaidi. Na tunapaswa kufanya kwazi kwa ushirikiano wa pamoja" alisema rais Obama.

Waziri wa Sheria wa Norway, Knut Storberget amesema mtu mmoja anatuhumiwa kuhusika na mauwaji ametiwa mbaroni.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Sekione Kitojo