VIENNA.polisi wanachunguza kuhusishwa watoto kwenye filamu za ngono | Habari za Ulimwengu | DW | 07.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIENNA.polisi wanachunguza kuhusishwa watoto kwenye filamu za ngono

Mmoja kati ya washtakiwa waliofikishwa mahakamani nchini Uhispania

Mmoja kati ya washtakiwa waliofikishwa mahakamani nchini Uhispania

Polisi nchini Austria wanachunguza kashfa ya kuwahusisha watoto katika filamu za ngono.

Takriban watu 2300 kutoka nchi 77 wanatuhumiwa katika kashfa hiyo.

Msemaji wa polisi mjini Vienna amesema kwamba washukiwa 23 wako nchini Austria zaidi ya mia sita wako nchini Marekani, washukiwa wengine 400 wako nchini Ujerumani na zaidi ya mia moja wako nchini Ufaransa.

Operesheni hiyo ya kuwasaka watu wanaohusika na kashfa hiyo ilianza tangu Julai mwaka jana.

Washukiwa walitambuliwa baada ukanda wa video kuonekana katika mtandao wa internet.

Msemaji huyo wa polisi amefahamisha kuwa mtandao huo unamilikiwa na kampuni moja ya Austria inayotoa huduma zake kutoka mjini London, Uingereza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com