VIENNA: El Baradei amealikwa kwenda Korea ya Kaskazini | Habari za Ulimwengu | DW | 24.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIENNA: El Baradei amealikwa kwenda Korea ya Kaskazini

Korea ya Kaskazini imemualika mkuu wa Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa IAEA,bwana Mohammed El Baradei kwenda Pyongyang kwa majadiliano kuhusika na mgogoro wa nyuklia wa nchi hiyo.Baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon mjini Vienna,El Baradei amesema ameukubali mualiko huo na atakwenda Korea ya Kaskazini hivi karibuni.Juma lililopita,serikali ya Pyongyang ilihakikisha kuwa itaachilia mbali mradi wake wa nyuklia na badala yake itapewa misaada mbali mbali katika sekta za nishati na uchumi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com