VICTORIA: Rais wa China, Hu Jintao, akamilisha ziara yake Afrika kwa ziara Ushelisheli. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VICTORIA: Rais wa China, Hu Jintao, akamilisha ziara yake Afrika kwa ziara Ushelisheli.

Rais wa China, Hu Jintao, leo anakamilisha ziara yake ya siku kumi na mbili ya mataifa manane barani Afrika kwa kuitembelea Ushelisheli.

Hii ndio ziara ya tatu ya rais huyo wa China, tangu alipotwaa madaraka mwaka elfu mbili na tatu.

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kisiasa kati ya China na Afrika.

Siku za karibuni uchumi unaokua wa China umekuwa ukitegemea zaidi mali ghafi kutoka barani Afrika.

Kabla ya ziara hiyo ya Rais Hu Jintao, serikali yake ilitangaza itayafuta madeni inayoyadai mataifa thelathini na matatu ya Afrika kutekeleza ahadi iliyotoa mwaka uliopita ya kusaidia kupiga jeki maendeleo ya bara hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com