1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwawanja mkuu wa olimpik tayari

16 Aprili 2008

Ujenzi umekamilika na waandishi habari walifunguliwa jana milango kuutembelea uwanja wa Olimpik wa Beijing.

https://p.dw.com/p/Dj8s

Mwenge wa michezo ya olimpik ya Beijing ukiwa umepita jana Pakistan, kwa safari yake ndefu hadi Beijing, uwanja mkuu wa michezo hiyo ulifunguliwa jana kwa mara ya kwanza kwa waandishi habari na vyombo vya habari vya kimataifa.

Maarufu kwa jina la "Bird's Nest"" nyumba ya ndege",uwanja huo wa kisasa kabisa uligharimu dala milioni 500.2.Ujenzi wa Uwanja huu ulianza desemba, 2003 na umemalizika wiki 14 baada ya wakati hasa uliopangiwa kumalizika.

►◄

Uwanja mkuu wa michezo ya Olimpik ya beijing uko tayari na jana ulifunguliwa rasmi milango yake kwa waandishi na vyombo vya habari vya kimataifa.zikisalia siku 113 tu kabla bunduki kulia kuanzisha mashindano ya kispoti na mashabiki wa olimpik kila pembe ya dunia kusahau misukosuko ilioandamana na mwenge wake, waandishi habari walijionea wafanyikazi wakipaka rangi mistari uwanja wa kukimbia (track).

Wamegundua pia kwamba baadhi ya viti 91,000 vya uwanja huo vinabidi kuchomekwa.

Wafanyikazi hao ambao hawakuonesha shauku ya kuzungumza na waandishi habari walisema tu "uwanja wa olimpik" ni maridadi ajabu.

Jua kali likipigana kupita katika ukungu uliotanda Beijing -hii ikikumbusha kazi kubwa bado inayopaswa kufanywa kusafisha hali ya hewa.

Kwani ,manunguniko yamesikika kutoka kwa baadhi ya wanariadha kuhusu moshi uliotanda juu ya anga la Beijing ambao waweza kuathiri afya zao.

Bingwa wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon, muethiopia Haile Gebreselassie, ameshaamua kutoshiriki katika mbio za marathon kutoklana na kuchafuka huko kwa hali ya hewa mjini Beijing.

Uwanja huu ulikuwa umalizike tayari mwaka jana 2007 pamoja na viwanja vyengine .Tarehe ya kumaliza ujenzi ikaahirishwa hadi Machi mwaka huu na halafu ikaahirishwa tena hadi kati ya mwezi huu.

Waandazi wa michezo ya beijing wamesema taabu ya kuundaa uwanja huu kwa kile kinachotarajiwa kuwa sherehe kubwa na shamra shamra za ufunguzi jioni ya August, 8 ndio sababu iliochelewesha mambo.

Ukamilishaji wa uwanja huu mkuu ndio kuakhirika pekee kukubwa katika mpango mzima wa majenzi ya vituo vya michezo hii ijayo ukilinganisha na matatizo ya Athens, kituo kilichopita cha Olimpik,2004.

Athens, rangi za mwisho uwanjani zikilakwa siku chache tu kabla michezo kufunguliwa rasmi.

Waandishi hao wa habari hawakuapewa maelezojuu ya mpango wa ufunguzi wa michezo utakavyokua,kwani kila kitu kimewekwa siri kubwa.Subiri tu ujionee.

Iliarifiwa Januari mwaka huu, kwamba wafanyikazi 2 walifariki wakati wa kazi za ujenzi. Maafisa walikanusha taarifa za vyombo vya habari kuwa eti hadi wafanyikazi 10 walifariki.

Mchezo wa kwanza utakaofanyika uwanjani ni mashindano ya kutembea haraka ya km 20 ijumaa hii.Mbio za marathon za jumapili hii za "Good luck Beijing marathon" zitamalizikia pia katika uwanja huu wenye umbo la nyumba ya ndege.

Mashindano ya riadha yaliopangwa kati ya Mei 22-25 ndio jaribio la kwanza barabara kujua iwapo utahimili vishindo vya wanariadha kutoka kila pembe ya dunia.

Wanariadha wake kwa waume wa Afrika wsamo basi kujinoa kwa Beijing 2008.