1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwaasi wa FDLR kutoka kwa Ujerumani

Dreyer, Maja23 Aprili 2008

Hivi jana, serikali ya Ujerumani imempokea rais wa Rwanda ambaye yuko safarini humu nchini. Gazeti la “Tageszeitung” la mjini Berlin ambalo linaangalia ziara ya rais Kagame wa Rwanda kutoka mtazamo mwingine.

https://p.dw.com/p/DnFr
Wanajeshi wa Ujerumani walisafiri hadi Kongo wakati wa uchaguzi. Vipi sasa jukumu la Ujerumani?Picha: AP

Gazeti la “Tageszeitung” linakumbusha kwamba serikali hii hii ya Ujerumani iliyomkaribisha rais wa Rwanda, inamvumilia kuishi nchini humu rais Ignace Murwanashyaka wa kundi la waasi wa Wahutu wa FDLR ambalo ni chama kirithi cha wale watu walioanzisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Mwandishi wa gazeti hilo Dominic Johnson ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Kiafrika, katika uchambuzi wake anailaani serikali ya Ujerumani kwa kumwezesha mwasi Murwanashyaka kuendesha ugaidi wake kutoka kwenye hifadhi yake hapa nchini. Ameandika hivi:


"Kuweka mpaka kati ya harakati za kisiasa na ugaidi ni vigumu sana. Tukiangalia malengo ya kisiasa ya kundi la waasi wa Kihutu wa FDLR, jina ambalo linamaanisha: “kundi la kidemokrasi la kuikomboa Rwanda”, malengo haya yanaonekana kuwa halali kabisa, hasa ni kuleta demokrasia zaida Rwanda. Kwa kweli lakini kundi hili linaendesha ugaidi mkubwa dhidi ya wakaazi wa kawaida wanaoishi Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.


Huko ndipo kundi la FDLR limeweka wanamgambo wake na kuendesha harakati za kijeshi karibu kabisa na mpaka wa Rwanda. Shahaba yao ni wazi, yaani kuanzisha vita nchini Rwanda na kuiangusha serikali ya rais Paul Kagame, ambaye ila kwa mkono mkali aliweza kuleta maendeleo makubwa katika nchi hii baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na kuijenga upya. Ukiangalia taarifa zinazochapisha na kundi la FDLR katika mtandao wa Internet karibu kila siku, unashindwa kuamini kwamba kundi hilo linataka kuelekea njia ya amani, hata ikiwa linasema hivyo mara kwa mara.


Ni kashfa kubwa kwamba viongozi wa FDLR wana uhuru wa kuendesha uwaasi wao kutoka Ujerumani kwa miaka mingi sasa bila ya kusumbuliwa. Lazima kashfa hiyo izungumzwe na hali hii isitishwe kama serikali ya Ujerumani inataka kuaminika pale inaposema kwamba inaunga mkono kuimarisha amani na kuleta maendeleo barani Afrika. Hata baada ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa zilimpiga marufuku rais wa FDLR Ignace Murwanashyaka kusafiri, lakini bado aliweza kuondoka Ujerumani kwenda Kongo kutembelea wanamgambo wake na hata kurudi Ulaya, safari yake ya mwisho ilikuwa mwaka 2006. Uchunguzi wa polisi dhidi yake ulisimamishwa mwaka uliopita kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi. Suali lakini ni, je, wachunguzi hao walichunguza wapi ili kupata kitu? Hawakuonekana katika eneo la Kongo Mashariki ambapo kundi la FDLR linatekeleza maovu yake.


Basi, muda umewadia Ujerumani ikubali jukumu lake katika kutuliza migogoro katika eneo la maziwa makuu. Kutumwa wanajeshi wa Kijerumani kuhakikisha uchaguzi wa amani hapo mwaka wa 2006 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kunaonyesha nia ipo kuimarisha usalama. Lakini nia hiyo lazima itekelezwe pia kivitendo hapa nchini."