1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uvutaji wa sigara hadharani wapigwa marufuku Ufaransa na sehemu za Ujerumani

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjSt

PARIS:

Hatua kadhaa zimechukuliwa za kupiga marufuku uvutaji sigara katika maeneo ya umaa katika nchi za Ufaransa na Ujerumani.

Kuanzia jumatano yeyote atakae kamatwa nchini Ufaransa akivuta sigara katika mkahawa atapigwa faini kati ya Euro 68 na 450.

Isitoshe mwenye biashara ambapo mtu huyo atakamatiwa watatozwa faini ya Euro 750 kwa kukiuka hatua hiyo.Na hapa Ujeruamani mikoa 6 kati ya yote 16 imepiga marufuku uvutaji wa sigara katika mikahawa na baa ambazo hazina nafasi maalum kwa ajili ya wavutaji sigara.Mikoa mitatu ya Ujeruamni ulianzisha utaratibu huo mwaka 2007.Mikoa mingine itaanza kutekeleza hatua zao hizi hapo baadae.Mwongozo kuhusu uvutaji sigara unatofautina kutoka mkoa mmoja hadi mwingine hapa Ujerumani.Wale ambao hupatwa na hatia hupewa faini za hadi Euro 2,500.