1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushirikiano Ujerumani -Afrika

13 Desemba 2007

Kikao maalumu kilifanyika mapema wiki hii mjini Frankfurt juu ya uwekezaji barani Afrika-kisa nini ?

https://p.dw.com/p/CbHX

Je, bara la Afrika ni bara la migogoro tu ? La, hasha, labda zamani.Kwani, sasa Afrika ni bara lenye kuanza kutoa matumaini na waafrika wenyewe kama mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Afrika mwishoni mwa wiki iliopita mjini Lisbon ulivyodhihirisha juu ya mkataba wa EPA wameanza kuzindukana kuwa wana turufu ya kiuchumi:nishati,migodi na hamu ya China kufanya biashara na Afrika.

Kwa muda sasa viwanda na makampuni ya Ujerumani yamekua nayo yakitia raslimali zao au kuekeza kati ya Cairo,Misri na Cape Town, Afrika Kusini.

Kwa lengo hilo,wiki hii ilifanyika mjini Frankfurt,Ujerumani warsha maalumu china ya kichwa :Siku ya uwekezaji barani Afrika.

Ilikua nafasi kwa muandishi wetu Daniel Pelz kujua ilikuaje hamu ya kuwekeza Afrika imeongezeka hivi sasa.kisa nini ?

Bw.Hanson Sindowe ni mtu anaesakwa mno siku hizi.Mwenyekiti huyo wa bodi ya nishati ya „Copperbelt Energy Corporation-ukanda wa shaba nchini Zambia amefunga mkataba.Shirika la maendeleo la Ujerumani-Dt.Entwicklungsgesellschaft-limechangia Euro milioni 8 kwa mradi wake.

Fedha hizo zitumike kukijenga katika muundo wa kisasa kiwanda chake. Kwani kampuni lake la nishati ambalo hadi sasa likieneza waya za umeme na kuuza mitambo ya kutoa umeme ya akiba endapo umeme umekatwa.Kampuni hili sasa lina azma ya kujitosa katika biashara ya kuzalisha umeme.

„Zambia ina uwezo mkubwa wa kiuchumi.Endapo kampuni lolote likwekeza huko,litaweza kuuza umeme huo hata katika maeneo jirani kwasababu kuna makampuni mengi yalio na upungufu wa umeme.“

Alisema Sindowe.

Miaka michache tu nyuma , wawekezaji wa Ulaya walimuangalia Hanson Sindowe kama ni muota ndoto na yakimpa kisogo.Na miaka michache nyuma, kampuni la mzambia huyo Sindowe lilikaribia kufilisika kwavile wawekezaji wa kignei walifunga virago na kumuacha mkono.

Sasa sura imebadilika na kama yeye Sindowe,anafurahia pia Bw.Jürgen Thumann, mwenyekiti wa Shirika la Ujerumani la wanaviwanda juu ya matumaini yanayonawiri barani Afrika.Ni bara la kila uwezekano .Anasema:

„Matokeo tangu ya kisiasa hatas ya kiuchumi wakati huu yanatia tamaa.Nafasi na uwezekanu wa kfanya biashara zinaongezeka. Chumi wa nchi nyingi za afrika umekuwa ukikua kwa kima cha hadi 6%.Zinasukuma mbele mageuzi na zinakuza masharti bora ya uwekaji raslimali.“

Asema mwenyekiti wa shirika la wanaviwanda wa ujerumani.

Hanson Sindawe anaelewa kwamba hamu inayooneshwa sasa na viwanda vya Ujerumani barani Afrika haitokani tu na kuwa uchumi wa Afrika sasa unaimarika:

Anasema:

„Serikali na nchi za Ulaya zimen’gamua sasa kwamba zina mshindani na mshindani huyo ni China.Ni dhahiri-shahiri kwamba China inasaka nafasi za kutia raslimali zake tena kwa kishindo kikubwa barani Afrika .Isitoshe, wachina wana muelekeo na utaratibu tofauti kujipatia kile watakacho kutokana na usuhuba wao wa kibiashara na Afrika.

Nchi za Ulaya zimegutuka sasa kwa kutambua zinabidi kurejea Afrika ama sihivyo zitakumbwa na matataizo baad aya China kutia mizizi yake huko.“- asema Sindowe.

Lakini hii sio rahisi hivyo.Kwani, china na Ulaya ni wapinzani 2 tofauti na wasio hirimu moja-anaeleza Katibu wa dola katika wizara ya uchumi ya Ujerumani: Bernd Pfaffenbach:

„kwa upande mwengine, huwezi kuilinganisha China na Ulaya.Ukizungumzia Ulaya na makampuni yake,hayo ni makampuni ya kibinafsi.Kwa upande wa China, nyuma yake ni serikali.Serikali inaweza kutia mkono mfukoni na kugawa kwa ukarimu,makampuni ya kibinafsi hayawezi kufanya hivyo…“

Uwezekano wa kutumia fedha hizo ni mkubwas.Nchi nyingi za kiafrika zina maliasili nyingi na kubwa .Nchi nyingi za afrika zinamiliki akiba kubwa ya dhahabu,madini ya uranium au mbao.Soko la simu za mkononi-handfys linakuwa na kuongezerka haraka mno.Na kuna mahitaji makubwa katika nchi za Afrika ya kujenga madaraja,barabara au viwanja vya ndege.Pia nchi nyingi za Afrika zinafanya mengi hivi sasa kuwavutia wa watiaji raslimali wa kigeni.

Wanatumai kwa njia hiyo,uchumi wao utakua na kuimarika na umasikini utapungua.Ghana kwa mfano ina azma hadi ifikapo mwaka 2015 kupunguza kwa nusu idadi ya masikini.

Lakini, waziri wa fedha Kwado Baah-Wiredu anaelewa kwamba shabaha hiyo haitawezekana kufikiwa kupitia raslimali zitakazotiwa nchini Ghana .Kwani, bado wezani wa biashara na nguvu za kiuchumi kati ya Afrika na Ulaya bado si sawa.