1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushiriki wa vyama vya Wakurdi wa Syria, katika mazungumzo ya Geneva

Admin.WagnerD27 Desemba 2013

Licha ya kuwepo kwa hali ya kutoaminiana kati ya wapinzani nchini Syria, hatimaye, vyama viwili vya kisiasa vyenye misimamo tofauti miongoni mwa watu wa kabila la Kurdi, vimekubaliana kuhudhuria mkutano wa amani, Geneva

https://p.dw.com/p/1Ahfc
Wakazi wa mji wa Marea nchini Syria walionusurika na mlipuko wa bomulililowekwa na vikosi vya serikali
Wakazi wa mji wa Marea nchini Syria walionusurika na mlipuko wa bomu lililowekwa na vikosi vya serikaliPicha: MOHAMMED AL-KHATIEB/AFP/Getty Images

Mkutano huo uliopangwa kujaribu kuleta upatanishi na kurejesha amani nchini Syria, kati ya serikali ya Bashar al Assad na wapiganaji wa upinzani, unatarajiwa kufanyika tarehe 22 Januari.

Ingawa maamuzi wapinzani hao wakikurdi kukubaliana kushiriki mazungumzo hayo ya amani huko Geneva yanatoa taswira ya mabadiliko ya kimwelekeo wa pande hizo mbili za watu wa kabila la kurdi zenye misimamo tofauti ya kisiasa, lakini bado kuna mashaka iwapo kama kweli makubaliano kati yao yatafanikiwa.

Mojawapo ya mikutano ya Umoja wa Mataifa,huko Geneva ya mikakati ya mazungumzo ya amani
Mojawapo ya mikutano ya Umoja wa Mataifa,huko Geneva ya mikakati ya mazungumzo ya amaniPicha: Getty Images

Baraza la watu wa Kurdistan linasemekana kuwa na elewano fulani na utawala wa Assad na lile baraza la taifa la Wakurdi liko karibu na makundi mengine ya upinzani.

Mkutano wa pili wa Geneva kuwa tegemeo la amani Syria

Aidha mkutano huo wa pili wa Geneva, umeshinikizwa na nchi za magharibi, ambazo ni Urusi, Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kiarabu, ambapo jumuiya ya kimataifa inatarajia mkutano huo utafungua njia ya kuundwa kwa serikali ya mpito na kumalizika kwa vita nchini Syria, ambavyo kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa Mataifa, tangu vita vimeanza, mpaka sasa kunasadikiwa , vimewauwa watu zaidi ya laki 1.

Hadi sasa hakuna maafikiano halisi yaliyofikiwa, kwamba iwapo serikali ya Syria itashiriki mkutano huo kwa mfumo wa mazungumzo ya pande mbili, yaani serikali na upinzani kwa ujumla au serikali na vikundi zaidi ya viwili vya upinzani.

Kwa mujibu wa mazungumzo yaliyofanywa na shirika la habari la IPS na wakurdi wenyewe, inaonyesha kuwa endapo kutakuwa na zaidi ya makundi mawili ya uwakilishi wa Wasyria katika mkutano huo wa Geneva, basi nao kama wakurdi watataka pia kushiriki kama kundi huru linalojisimamia.

Vikosi vya serikali ya Syria vikiwa katika doria mjini Al Mseifri,kusini mashariki mwa mji wa Aleppo
Vikosi vya serikali ya Syria vikiwa katika doria mjini Al Mseifri,kusini mashariki mwa mji wa AleppoPicha: picture alliance/dpa

Mwenyekiti mwenza wa Chama cha upinzani cha watu wa magharibi, Abdulsalam Ahmed, aliliambia shirika la habari la IPS kuwa mazungumzo hayo ya Geneva, yatakuwa kama chanzo cha matarajio ya baadae ya Syria.

Abdulsalam Ahmed alisema hayo, baada ya kumaliza mazungumzo mazito ya siku nane mfululizo na Chama cha KNC, wanacho tofautiana nacho kimsimamo, ambapo walikuwa na mazungumzo kupanga mikakati ya ushiriki wao katika mkutano wa Geneva, wakiwa na msimamo wa pamoja kwa kuongozwa na mkataba wa kuunganisha nguvu kwa ajili ya kuliongoza taifa hilo.

Umuhimu wa Wakurdi katika Taifa la Wasyria

Abdulsalam Ahmed aliongeza kuwa, wao kama wakurdi, wana umuhimu mkubwa, katika uwakilishi kwenye mkutano wa Geneva na kuonya kuwa machafuko ya Syria hayawezi kutatuliwa bila kuzingatia uwepo wa Wakurdi ambao wanadai wapatiwe haki zao kama kabila la pili kwa ukubwa nchini humo na kwamba jumuiya ya kimataifa lazima ielewe hivyo na wawape fursa ya kuwa muhimili muhimu katika mazungumzo hayo, kwa lengo la kuleta usawa na amani katika nchi hiyo kwa siku zijazo.

Hali ya mambo katika taifa hilo la Syria lenye mgawanyiko mkubwa na kutoaminiana wenyewe kwa wenyewe, limewafanya Watu wa kabila la Wakurdi kutokuwa na imani na chama chochote kinachowawakilisha kisiasa .

Mwandishi: Diana Kago/IPS
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman