1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalimishaji silaha Ivory Coast kuanza Desemba 22

Mohammed Abdul-Rahman2 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVk0

Korhogo-Ivory Coast:

Majeshi ya serikali ya Ivory Coast na waasi nchini humo wanaoithibiti sehemu ya kaskazini, wataanza zoezi la kuwavua silaha wapiganaji wao tarehe 22 mwezi huu, kabla ya kuundwa jeshi jipya la taifa. Taarifa hiyo ilitangazwa na mpatanishi, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Burkina Faso Djibril Bassole, ambaye nchi yake ilikua mwenye wa mazungumzo kati ya pande hizo mbili mwezi Machi, ambapo zilikubaliana kuiunganisha tena Ivory Coast iliogawika pande mbili baada ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe 2002 hadi 2003.