1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama wa ndani wazua majadiliano Ujerumani

Sekione Kitojo
9 Januari 2017

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamezungumzia mjadala kuhusu usalama wa ndani baada ya shambulio la mjini Berlin, je Putin anahusika katika kushawishi mkondo wa uchaguzi nchini Marekani, na miaka kumi ya Smartphone.

https://p.dw.com/p/2VVb9
Berlin Wiedereröffnung Weihnachtsmarkt nach Anschlag mit LKW
Vizuwizi katika soko la krismass mjini BerlinPicha: DW/F. Hofmann

 Kuhusiana  na  mjadala wa usalama  wa  ndani nchini  Ujerumani , mhariri  wa  gazeti  la  Rhein-Neckar-Zeitung  la  mjini  Heidelberg anaandika:

Hali  haionekani  kabisa  kuwa  ni ya  usalama  wa  kutosha. Kwasababu  hakuna  hadi  sasa  mwelekeo  wa  wazi, ambao ungewezekana  kuzuwia shambulio dhidi  ya soko  la  krismass  mjini Berlin, iwapo  vizuwizi  vya  saruji  vilivyowekwa  hivi  sasa vitaondolewa. Kutumia  hatua  hizo  anaona  mhariri  kuwa  ni muhimu  zaidi  kuliko  kuweka  sheria  mpya  na  mifumo. Ni  vizuri basi  kutumia  sera zilizopo za  usalama , pamoja  na  sheria  zilizopo.

CDU Parteitag in Essen - Tauber
Katibu mkuu wa CDU Peter TauberPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Gazeti  la  Landeszeitung  la  mjini  Lüneburg  likizungumzia  kuhusu mada  hiyo  ya  usalama  wa  ndani  linaandika.

Baadhi  ya  wanasiasa  hisia  zao  tayari  ziko  katika  uchaguzi mkuu  tu.  Hali  hiyo  pia  iko  kwa  wananchi  wengi. Wanasiasa wameanza   kujiingiza  rasmi  katika  mjadala  kuhusu  shambulio  la kigaidi mjini  Berlin  hususan  katibu  mkuu  wa  chama  tawala  CDU Peter Tauber Sahra Wagenknecht  na  Frauke Petry  wakiwa  ni watu  wawili  ambao  wanapalilia  siasa  kali  za  mrengo  wa kulia.Lakini  wawakilishi  hawa  wa  wananchi  hawapaswi kushangaa , wakati  ndugu  za  watu  waliopoteza  maisha  na kujeruhiwa  katika shambulio  la  mjini  Berlin  wanahisi  kwamba wanasiasa  wamewatupa  kando. Tauber  na  wenzake  wanapaswa hatimaye kutambua  , kwamba  siasa  za  kuwagawa  wananchi  ama siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia  hazi  katika  mjadala  huu.

Uchaguzi nchini Marekani

Kuhusu uchaguzi  wa  Marekani  na  udukuzi  wa  Urusi katika uchaguzi  huo , mhariri  wa  gazeti  la  Frankfurter Allgemeine Zeitung anaandika:

Ni  kwa  kiasi  gani athari za  wizi,  udukuzi pamoja  na  wapi  taarifa hizo  za  udukuzi  zimepelekwa  katika  uchaguzi  mkuu  wa  rais nchini  Marekani  zilichangia  katika  kubadilisha  matokeo, ni  suala ambalo  haliwezi kupimwa. Lakini  iwapo  itaweza  kuthibitishwa, kwamba  nguvu  kutoka  nje  zilichangia  kuingilia  kati mchakato  wa kidemokrasia  nchini  Marekani, matokeo  yake yanaonekana  dunia nzima. Na kwa  hakika   hata Trump  anaweza  kumridhia  Putin. Hakuna  mtu  ambaye  angeweza bila  shaka  kukubali uhalali wa Trump. Iwapo kulikuwa  na  operesheni  kama  hiyo,bila ya  kupata idhini  kutoka  juu, basi  shirika  la  kijasusi  la  Urusi  linapaswa kupongezwa  kwa  kazi ya  mapinduzi lililofanya.

Sprachsteuerung
Smartphone iliyoleta mabadiliko dunianiPicha: picture-alliance/dpa/A. Heinl

Smartphone:

Na  simu  za  mkononi  -Smartphone- zinatimiza  miaka  10, mhariri wa  gazeti  la Der tagesspiegel  anaandika.

Simu  za  mkononi  za  Smartphone  ni  msingi  wa  sekta  mpya  ya kiuchumi. Katika  bara  la  Ulaya , baadhi  ya  watu  wanajiuliza, iwapo  chombo  hicho  kinawalazimisha  watu  kuingia  katika utumwa  wa  kimamboleo na  iwapo   watu  wanaweza  kujiepusha nao. Katika  nchi  zinazoendelea  simu  hizo  zimewaingiza  watu wengi  katika  hali  ya  kujitegemea  na  kutatua  matatizo   halisi. Kwa  kutumia  app wakulima  wadogo  wadogo  wameweza  kujifunza masuala  ya  kilimo, na  kuweza  kuweka  mashamba  yao  katika hali  bora  zaidi. Wafugaji  wameweza  kulipa  malipo  yao  ya  bima ya  majanga  kupitia  simu  zao za  mkononi, wakati  ukame  ukiwa umeendelea  kwa  muda  mrefu. Iwapo  watu  wanakabiliwa  na  njaa katika  maeneo  kame, wameweza kutuma  taarifa  kwa  serikali  ili  kupata msaada  kupitia  simu  zao za  mkononi.

 

Mwandishi:   Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Yusuf Saumu