1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasimamisha luteka za kijeshi

Admin.WagnerD4 Machi 2014

Rais Vladimir Putin wa Urusi amewaamuru wanajeshi wake waliohusika katika luteka za kijeshi ambazo baadhi zikifanyika karibu na Ukraine warudi kwenye kambi zao. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wake Dmitri Peskov.

https://p.dw.com/p/1BJH9
Wanajeshi wa Urusi katika jimbo la Crimea, Kusini mwa Ukraine
Wanajeshi wa Urusi katika jimbo la Crimea, Kusini mwa UkrainePicha: Reuters

Luteka hizo zilizokuwa na lengo la kuonyesha utayarifu wa majeshi ya Urusi, ni jambo lililozitia wasiwasi serikali za nchi za magharibi baada ya Urusi kutuma mamiaya wanajeshi katika eneo lina Ukraine la Crimea ambako wakaazi wake wengi ni wenye asili ya urusi, ikiwa ni baada sya kuangushwa rais wa zamani Viktor yanukovich na wapinzani wanaoelemea upande wa magharibi.

“Luteka hizo zilizoanza wiki iliopita zitamalizika kama ilivyo pangwa,"hivyo ndivyo alivyoeleza msemaji huyo

Haikuweza kufahamika wazi ikiwa hatua hiyo ya rais Putin ni jaribio la kuitekea baadhi ya wito wan chi za magharibi kuutuliza mzozo huo ambao umeupa mtihani mkubwa mustakbali wa Ukraine .

Kerry atua mjini Kiev

Hatua hiyo imekuja wakati Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akielekea Kiev kwa mazungumzo na utawala mpya ambao umeshutumu Urusi kwa uvamizi wa kijeshi. Ikulu ya Urusi ambayo haiutambui uongozi mpya mjini Kiev inashikilia kwamba hatua yake ni kwa ajili ya kuwalinda mamilioni ya Warusi wanaoishi Crimea.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amewasili mjini Kiev kuiunga mkono serikali mpya ya Ukraine
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amewasili mjini Kiev kuiunga mkono serikali mpya ya UkrainePicha: Reuters

Katika mjadala kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana , Balozi wa Urusi alisema kiongozi wa aliyeondolewa madarakani Viktor Yanukovich aliiandikia barua Urusi kuiomba ijiingize kijeshi kurejesha amani , sheria na utengamano.

Takriban wanachama wote wa baraza hilo waliitaka Urusi kuyaondoa majeshi yake katika ardhi ya Ukraine, wito ulioungwa mkono hata na mshirika wake China.

Mjini Washington, rais Barack Obama wa Marekani aliita hatua ya Urusi kujiingiza kijeshi katika jimbo, la Crimea kuwa ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa. Obama akalitaka bunge kuidhinisha mpango wa msaada kwa serikali ya Ukraine na kutoa tena kitisho kwamba Marekani itachukua hatua kuiadhibu Urusi kiuchumi na kuitenga kidiplomasia.

Obama aikosoa tena Urusi

Hata hivyo afisa mmoja wa Ikulu ya Urusi mjini Moscow ameionya Marekani akisema vikwazo dhidi ya Urusi akisema pindi ikifanya hivyo, mfumo mzima wa fedha wa Marekani utaporomoka na Urusi itatafuta njia mbadala ya kutoitegemea marekani hata kidogo.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin
Rais wa Urusi, Vladimir PutinPicha: REUTERS

Wakati huo huo pamoja na kwamba hali ya mambo ni shwari kwa kiasi fulani katika jimbo la Ukraine la Crimea,mapema leo watu waliokuwa na silaha wanaoiunga mkono Urusi huko Crimea walifyatua risasi hewani kuwatawanya wanajeshi wapatao 300 wa Ukraine ambao waliizingira kambi ya jeshi la anga ya Belbek,wakidai warejeshwe kazini. Wanajeshi kadhaa wa Urusi walionekana wakiangalia tu tukio hilo .

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, afp, ap

Mhariri:Saumu ,Yusuf