1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi Yaonywa Isiingilie Mzozo wa Ukraine

8 Aprili 2014

Hali inatisha mashariki ya Ukraine ambako wanaharakati wanaoelemea upande wa Urusi wamejitangazia "Jamhuri ya Donetsk". Urusi imeonya dhidi ya hatari ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe Ukraine ikiingilia kati.

https://p.dw.com/p/1BdeX
Mapigano yamezuka kati ya wabunge wa Ukraine mjini KievPicha: Reuters

"Waasi wanaobeba silaha,wanaopigania kujitenga maeneo ya mashariki,walioyavamia majengo ya serikali wataandamwa kuambatana na katiba na sheria na kulinganishwa na magaidi na wahalifu" amesema hayo rais wa mpito Olexandre Turtchinov.

Akihutubia bungeni hii leo rais Turtchinov amesisitiza jeshi halitoshamiri silaha dhidi ya watu wanaoandamana kwa amani katika wakati ambapo wanaharakati wanaoelemea upande wa Urusi wanadhibiti majengo ya serikali maashariki ya nchi hiyo nayo Urusi inaonya dhidi ya hatari ya kuripuka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Rais Turtchinov amethibitisha silaha na maguruneti yametumiwa dhidi ya vikosi vya wanajeshi waliowekwa kulinda majengo ya serikali katika mji wa Kharkiv na kwamba wanajeshi kadhaa wamejeruhiwa. Ameelezea matumaini yake kuyaona majengo ya setrikali yakikombolewa haraka huko Lougansk na shughuli za tawala kuendelea kama kawaida katika mji wa Donetsk ambako wanaharakati wanaoelemea upande wa Urusi wametangaza "jamhuri yao".

Urusi imeitaka Ukraine iache maandalizi ya kuingilia kijeshi katika maeneo hayo ya mashariki. Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Urusi inahoji watumishi wa shirika la kibinafsi la Marekani wanashiriki katika opereshini hizo.

Jumuia ya Kimataifa itakutana Haraka kuzungumzia Ukraine

Katika wakati ambapo Urusi inaonya dhidi ya hatari ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe katika maeneo ya mashariki ya Ukraine,jumuia ya kujihami ya NATO imeitolea wito Moscow iwarejeshe nyuma wanajeshi wake waliokusanywa karibu na mpaka wa nchi hizo mbili.

Putin Rede FSB 07.04.2014 Moskau
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Reuters/Mikhail Klimetyev/RIA Novosti

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amezungumza kwa simu na waziri mwwenzake wa urusi Sergei Lavrov na kumuonya Washington inafuatilizia kwa wasi wasi mkubwa yanayotokea Mashariki ya Ukraine.Waziri Kerry ameitaka Urusi ijitenganishe na wanaopigania kujitenga eneo hilo,wanaofanya fujo na kuchochea mizozo.

Mawaziri hao wawili wamezungumzia umuhimu wa kuitishwa mkutano kati ya Ukraine, Urusi, Marekani na Umoja wa Ulaya ili kumaliza mivutano.

Bendera za Urusi zapepea Mashariki ya Ukraine

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinemeir anasema:"Tunabidi tufanye bidii kuisaidia Ukraine kiuchumi na kisiasa. Juhudi hizo hazitafanikiwa mtengano ukitokea nchini humo.

Pro-russische Demonstration in Charkiw 05.04.2014
Waandamanaji wanaoelemea upande wa Urusi wanaandamana karibu na sanamu la mtunzi wa kirusi Vladimir MayakovskyPicha: picture-alliance/dpa

Yadhihirika kana kwamba hilo ndilo linalotokea;bendera za Urusi zinapepea katika majrengo yote yanayokaliwa na waasi mashariki ya Ukraine.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/Reuters

Mhariri: Josephat Charo