1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yailaumu Marekani kuhusu Kosovo

21 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DSIm

MOSCOW:

Urusi imeikosoa Marekani kwa mipango yake ya kuipa silaha Kosovo.Waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa mipango ya serikali ya Marekani inakiuka azimio la Umoja wa Mataifa ambalo linaruhusu tu silaha kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa ya Kosovo.Vyombo vya habari vya Urusi vinasema kuwa serikali ya Moscow inapanga kuchukua suala hilo katika kikao maalum na NATO.Washington imepinga wasiwasi uliopo kuwa msaada wa kijeshi kwa taifa changa la Kosovo kutahatarisha usalama wa eneo hilo.Ikulu ya White House ,kupitia taarifa ,imesema kuwa Kosovo ina haki ya kuwa na jeshi japo dogo chini ya mpango wa kujitegemea ulioratibiwa na mjumbe wa umoja wa Mataifa,Martii Ahtisaari.